Home Habari za Yanga Leo PACOME ATOA KAULI HII…AMTAJA MSINDO

PACOME ATOA KAULI HII…AMTAJA MSINDO

Pacome na Habari za Yanga

KIUNGO mchezeshaji wa Yanga, Muivory Coast Pacome Zouzoua amepanga kuwa na msimu mzuri katika msimu ujao, ikiwemo kuendelea kuipa mataji timu hiyo.

Nyota huyo ni kati ya wachezaji walitoa mchango mkubwa katika kikosi hicho, ikiwemo kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kuifikisha timu katika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Pacome alisema kuwa majeraha ya goti aliyoyapata katikati ya msimu huu, yameharibu mipango yake aliyoiweka.

Pacome alisema kuwa, majeraha hayo yamesababisha ashindwe kuonyesha kiwango chake bora alichonacho, akiwa na Yanga aliyojiunga nayo msimu huu.

Pacome aliumia zaidi kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC,  baada ya kukutana na Beki wa kushoto wa klabu hiyo, Pascal Msindo ambapo alitolewa nje katika kipindi cha kwanza na alikaa nje kwa muda mrefu kabla ya kurudi ndani ya uwanjani mwishoni mwa msimu.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara wamemaliza msimu wa 2023/24 wakiwa namba moja na pointi 80 kibindoni baada ya mechi 30.

Pia wana taji la CRDB Federation Cup ambalo walitwaa mbele ya Azam FC kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Hii inakuwa ni  mara ya tatu kwa Yanga kuchukua kombe hilo mfululizo, na mara ya  nne tangu kurejea  kwa mashindano hayo mwaka 2015. Lakini klabu hiyo imetwaa taji la FA mara 8 na kuwa namba moja kwa timu zinazoongoza kuchukua.

SOMA NA HII  YANGA NI MIPESA TU...HII HAPA JUMLA YA FEDHA WATAZOVUNA KWA KUINGIA FAINAL TU...