Home Habari za Simba Leo MA “GIANTS” KOMBE LA SHIRIKISHO… SIMBA AWE MAKINI…LASIVYO!

MA “GIANTS” KOMBE LA SHIRIKISHO… SIMBA AWE MAKINI…LASIVYO!

Habari za Simba leo

SHIRIKISHO kwa moto sana, ujue sio Simba tu aliyedondokea huko baada ya kufana vibaya kwenye Ligi msimu uliomalizika, ila vilabu vingi vikubwa barani Afrika, vilivyokuwa Ligi ya Mabingwa msimu ulioisha vimejikuta vikiangukia hadi kombe la Shirkisho.

Bila shaka kwa mashabiki wa Simba hawatakiwi kabisa kukata tamaa, na kujioni wameenda kwenye mashindano ya walioshindwa “Looser” kama ambavyo mashindano hayo yamekuwa yakizungumzwa kama utani na baadhi ya waandishi au mashabiki.

Klabu ya Simba na Uongozi wake hawataki kuvunjika moyo kucheza kombe la Shirkisho kwani kuna vigogo wenzao walikuwa nao Ligi ya Mabingwa na wamekutana huko, hivyo bado ngoma ngumu bila usajili wa wachezaji wa maana huenda hata kufika hatua waliyozoea ya robo fainali itakuwa ni ngumu.

MA”GIANT” WA KOMBE LA SHIRIKISHO

Msimu wa 2024/25 kwenye Kombe la Shirkikosha Afrika kuna miamba haswa, tena timu zenye viwango vikubwa, ukijumlisha na uzoefu wa vilabu hivyo kwenye mashindano ya kimataifa, basi moto utawaka, kwa ufupi unaweza kusema Kombe la Shirikisho ni kama Ligi ya Mabingwa tu utofauti ni jina.

1. Zamalek SC- Misri
2. Wydad Athletic Club- Morocco
3. Asec Mimosas- Ivory Coast.
4. RS Berkane- Morocco
5. AS Vita Club- DR Congo
6. CS Sfaxien- Tunisia
7. Zesco United- Zambia
8. Etoile du Sahel- Tunisia
9. Coton Sport de Garoua- Cameroon
10. USM Alger- Algeria
11. Premeiro de Agosto-Angola
12. Asante Kotoko- Ghana
13. Hearts of Oak- Ghana
14. Stade Malien- Mali
15.Real Bamako- Mali
16. Kaizer Chiefs- Afrika Kusini
17. Vipers SC- Uganda
18. Power Dynamos- Zambia.

SOMA NA HII  AHMED ALLY : MASHABIKI WANAHAKI KUSEMA HAWAMTAKI MATOLA...AFUNGUKA MSIMAMO WA KLABU ...