Home Habari za Yanga Leo AZIZ KI ANATESTI MITAMBO…MKATABA UMEISHA YANGA..KAIZER CHIEFS & MAMELODI ZAHUSISHWA

AZIZ KI ANATESTI MITAMBO…MKATABA UMEISHA YANGA..KAIZER CHIEFS & MAMELODI ZAHUSISHWA

Aziz ki yanga

JUNI 14, ndiyo mwisho wa mkataba wa Kiungo Aziz Ki pale mitaa ya Jangwani, ambapo tayari kumeanza kusikika harufu za mchezaji huyo kutimkia kwingine, ambapo anahusishwa zaidi na Mamelodi, Kaizer Cheifs za Afrika Kusini na timu za kutoka Morocco.

Hata hivyo kwa dalili zinazoonekana, kuna uwezekano mdogo kwa Aziz Ki kuachana na Yanga na hivyo anaenda kusaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao na hata mwingine zaidi.

Sababu ya kwanza ambayo inaonekana ina nguvu kubwa katika kumshawishi Aziz Ki abakie Yanga ni mzigo ambao bila shaka timu hiyo itamwekea mezani katika mkataba mpya kwa maana ya dau la kusaini mkataba pamoja na mishahara na stahiki nyingine kama vile posho na bonasi.

Aziz Ki anahitaji mshahara wa dola 20,000/= sawa na Tsh Mil 50, pamoja na dau lake la usajili ambapo kwa mujibu wa Transfermarkert, nyota huyo ana thamani ya Euro 2,500,000/= sawa na Tsh Milioni Mia Saba na Kumi na Mbili (Tsh m712/=)

Yanga haipo kinyonge na kwa sasa mzigo upo, hivyo haiwezi kukubali kumkosa mchezaji muhimu na tegemeo kisa kiasi cha fedha, ambacho inaweza kukifikia au kukikaribia kupitia kwa vyanzo vyake hasa mfadhili na wadhamini ilionao.

Inawezekana Aziz Ki akaahidiwa dau kubwa huko nje, pia likaambatana na kodi kubwa pamoja na gharama kubwa za maisha zaidi ya zile za hapa, hivyo akaamua kuchukua mzigo wa Yanga ambao hatoutumia sana.

Ni mchezaji ambaye hana presha kubwa ndani ya timu hiyo kwa sasa na ni staa mkubwa kulinganisha na huko kwingine anakoweza kwenda ambako atalazimika kuanza upya.

Lakini hapa Tanzania jamaa ana uhuru mkubwa wa kufanya starehe bila bughudha yoyote na inasemekana tayari ameshakamata hisia za mtoto mmoja mkali wa Kibongo ambaye hali halali kwa ajili yake.

Anachokifanya kwa sasa ni kupandisha tu thamani yake ili Yanga itoe kibunda cha uhakika maana akiwahakikishia moja kwa moja kuwa anabaki, wanaweza kumchukulia poa na kutompatia kile anachokihitaji.

SOMA NA HII  KUNA MAXI NZENGELI MMOJA TU YANGA...SI PACOME, CHAMA WALA NANI