Home Habari za Yanga Leo USIKU WA TUZO ZA BMT…YANGA WAZIKIMBIZA SIMBA & AZAM FC

USIKU WA TUZO ZA BMT…YANGA WAZIKIMBIZA SIMBA & AZAM FC

Habari za Yanga- Injinia Hersi Tuzo
Rais wetu Eng. Hersi Said akikabidhiwa Tuzo ya klabu bora ya kiume mwaka 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance, Kaimu Mkeyenge.

USIKU wa Tuzo za Baraza la Michezo  Taifa, ulifana sana ambapo klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa Tuzo ya Timu Bora ya Kiume ya Mwaka 2023 kwa ngazi ya vilabu.

Ndani ya mwaka huo Yanga ilitwaa Ubingwa Ligi kuu, Ubingwa FA, Ngao ya Jamii sambamba na kufanikiwa kufika fainali ya kombe la Shirikisho Afrika.

Pia Timu ya Taifa ya Wanaume ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshinda Tuzo ya Timu Bora ya Kiume Mwaka 2023 kwa ngazi ya taifa kwenye tuzo zinazotolewa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT).

Washindi wengine wa tuzo hizo za BMT  2023

Tuzo ya Mwandishi bora wa Michezo wa kiume imeenda kwa Hussein Shafih kutoka Shirika la Utangazaji TBC

Mwandishi bora wa Michezo wa kike ni Fatma Chikawe kutoka Azam Media

Ahmed Arajiga Mwamuzi bora wa kiume wa Mwaka tuzo za BMT

Mwamuzi bora wa kike wa Mwaka ni Pendo Njau

Tuzo ya mwanamichezo bora chipukizi wa kiume imekwenda kwa Romeo ambaye ni mkali wa kuogolea.

Mwanamichezo bora wa kiume mwaka 2023 ni bondia Yusuph Changalawe.

Tuzo ya Timu Bora ya klabu kwa upande wa wanawake, imekwenda kwa JKT Queens.

Mwanamichezo bora wa kike mwaka 2023 ni bondia bondia Grace Mwakamele.

Timu ya Taifa ya Wanawake upande wa kriketi imetwaa Tuzo ya Timu Bora ya Taifa upande wa Wanawake.

Bondia Grace Mwakamele ndiye Mwanamichezo Bora wa kike mwaka 2023

Vosta Isaya Lengonela wakati akipokea tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka kwa wenye ulemavu.

Tuzo ya heshima kwa nahodha wa zamani wa Taifa Stars ambaye ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

Mwanamichezo bora wa kike kutoka shuleni ni Happiness Fabian Kongoka kutoka Kapuya Sekondari, Kaliua Tabora.

Tuzo ya mwanamichezo bora wa kiume kutoka shuleni imekwenda kwa Agape Mwenda.

SOMA NA HII  WAPINZANI WA YANGA CAF KUTUA BONGO LEO....KOCHA WAO AITAJA SIMBA MWANZO MWISHO..