WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro, ameipongeza Yanga kwa mafanikio makubwa, chini ya Rais wa klabu hiyo, injinia Hersi Said, akiwataka Simba Kuondoa migogoro iliyopo ndani ya klabu yao ili kufikia mafanikio ya malengo yao.
Dkt Ndumbaro ambaye pia ni mwanachama wa Simba SC, alisema kwamba Yanga na Azam FC zimeongeza ubora wao, ila Simba hajashuka kiwano, lakini anashangaa ni kwanini kumekuwa na migogoro katika klabu hiyo.
“Siamini kama Simba ni mbaya, isingefika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, shida ninayoiona ni ubora wa Yanga na Azam, hivyo ijifunze na ikajipange upya, shida ya Simba na Yanga mojawapo ikiwa vizuri nyingine inaibua migogoro, hivyo zinatakiwa kubadilika,”
Hata Hivyo Dkt Ndumbaro aliwataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga wajitahidi kumlinda Injinia Hersi kwa mafanikio wa klabu yao na maendeleo ya mpira wa miguu nchini.