Home Habari za michezo MBIVU NA MBICHI YANGA KUJULIKAMA JTATU….WATAKAOPEWA ‘THANK YOU’ HAWA HAPA…

MBIVU NA MBICHI YANGA KUJULIKAMA JTATU….WATAKAOPEWA ‘THANK YOU’ HAWA HAPA…

tetesi za usajili Yanga leo

Taarifa kutoka katika uongozi wa Klabu ya Young Africans zinabainisha kwamba, Julai Mosi, mwaka huu itafahamika rasmi kikosi cha timu hiyo kitakuwaje kuelekea msimu ujao.

Katika kukifahamu rasmi kikosi cha Yanga kuelekea msimu ujao, wachezaji wapya waliosajiliwa, walioongezewa mikataba na wale walioondoka watawekwa wazi.

Julai Mosi ambayo itakuwa Jumatatu ya wiki ijayo, mbali na kujulikana usajili mzima wa kikosi cha timu hiyo, pia itafahamika kambi itakuwa wapi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, amesema: “Julai Mosi ndiyo siku ambayo sisi Yanga tutangaza kambi ya timu yetu itakuwa wapi, pia tutaweka bayana kikosi chetu cha msimu ujao kwa maana ya kuwataja wachezaji walioondoka, walioongeza mikataba na wapya waliosajiliwa.”

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinadai kuwa , miongoni mwa wachezaji watakopewa ‘Thank You’ ni pamoja na Farid Musa, Joyce Lomalisa, Kennedy Musonda, Zawadi Mauya, Davis Nkane na Gift Fred.

Aidha inasemekana kuwa Yanga Day Mwaka huu huenda ikawa kati ya tarehe 29/7 na tarehe 3 mwezi wa nane.

 

SOMA NA HII  USIKAE KINYONGE WAKATI KUNA BONASI YA MIL 10 ZA BUREE KUTOKA MERIDIANBET....