Home Habari za michezo TETESI ZA USAJILI:-KITASA HIKI HAPA KINATUA SIMBA…..JAMAA NI BALAA TUPU πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯…

TETESI ZA USAJILI:-KITASA HIKI HAPA KINATUA SIMBA…..JAMAA NI BALAA TUPU πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯…

Tetesi za Usajili Simba

Imeripotiwa kwamba, Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo na beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Burkina Faso na FC Lupopo ya DR Congo, Valentin Nouma (24) kwa ajili ya kuipata huduma yake.

Simba ambayo imepanga kujiimarisha zaidi kuelekea msimu ujao, inaamini kwamba beki huyo anayecheza kikosi cha Burkina Faso sambamba na kiungo wa Yanga Stephane Aziz Ki, anaweza kuwa mtu sahihi kwao.

Uamuzi wa Simba kusaka beki wa kushoto umekuja baada ya kumtumia kwa muda mrefu nahodha wao, Mohamed Hussein β€˜Tshabalala’ ambaye anaonekana mpinzani wake ameshindwa kupatikana.

Katika hatua nyingine, Crescentius Magori wiki hii ameenda Zambia kwa ajili ya mazungumzo na wachezaji wawili ambao ni wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia.

Magori alitua Zambia jumatatu Juni 10 ili kuwatazama wachezaji hao kwenye mchezo dhidi ya Tanzania, Simba SC inasuka kikosi kurejesha ufalme.

SOMA NA HII  MSAIDIZI WA KOCHA WA AL AHLY APETA NAFASI YA UKOCHA SIMBA..TRY AGAIN AFUNGUKA ...