Home Habari za Yanga Leo MAPYA YAIBUKA SAKATA LA CLATOUS CHAMA…HAPOKEI SIMU ZA YANGA

MAPYA YAIBUKA SAKATA LA CLATOUS CHAMA…HAPOKEI SIMU ZA YANGA

Habari za Yanga, Clatous Chama

TAARIFA kutoka chanzo cha kuaminika Simba SC, kinaeleza kwamba Sakata la Clatous Chama kujiunga na Yanga bado ngoma ni mbichi, kwa sababu Chama hajafurahishwa na Yanga kumtambulisha hali ya kuwa yeye alikuwa kwenye mazungumzo na Simba.

Iko hivi, ule mkataba ambao unaonekana kwenye ile picha ambayo Klabu ya Yanga ilimtambulisha Clatous Chama kuwa ni mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo ulikuwa ni mkataba wa makubaliano ya awali.

Kitaalamu tunaita Pre contract ambao ulisainiwa kati ya mchezaji na Uongozi wa Yanga mwezi wa tatu mwaka huu huku mchezaji akisubiria kutamatika kwa mkataba wake na Simba ambao ulifika tamati June 30 mwaka huu, na kuona kama ataboreshewa maslahi ya mkataba mpya na timu yake ya sasa ambayo ni Simba.

Baada ya mkataba wa Simba na Chama kumalizika Uongozi wa Yanga ulimuingizia pesa za usajili Clatous Chama ili aende akasaini mkataba kamili na wao jambo ambalo aliwaambia wasubirie bado anamazungumzo na Uongozi wa timu aliyopo kwa sasa ambayo ni Simba.

Endapo kama wakishindwana basi atawarejea wao, baada ya mazungumzo marefu ambayo hayakupata muafaka na uongozi ndio Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji akamuita Chama Dubai kwa mazungumzo marefu sana.

Kisha akapewa mahitaji yote ya kimkataba ambayo alikuwa anahitaji kutoka Simba na maboresho ya mshahara na pesa za usajili zikaboreshwa pia Mwamba akachukua mzigo kutoka kwa tajiri Mo akaweka kibindoni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo kingine inaelezwa kwamba MO Dewji alimpa pesa Chama.

“Alimwambia atamlipa mshahara milioni 40 na signing fee Mil 250 na Chama akakubali hii Juzi Juzi na MO akampa motisha kiasi Cha fedha amalize mahitaji yake.”

CHAMA ikabidi awasiliane na Uongozi wa Yanga kuupa taarifa kuwa yeye anasalia ndani ya Simba ameshamalizana na Tajiri hivyo hatoweza kujiunga kwenye timu yao na kuwataka awarudishie pesa zao.

Uongozi wa Yanga ukaona wanazidiwa kete wakaamua kuposti hizo picha ambazo walipiga kitambo wakati wanamsainisha mkataba wa awali kisha kuwatangazia mashabiki kuwa wameshamsajili CHAMA jambo ambalo sio kweli Chama bado hajasaini mkataba rasmi na Yanga.

Kinachoendelea kwa sasa CHAMA amewaambia Uongozi wa Simba anataka kubakia kucheza Simba hivyo warudishe pesa ya Yanga aliyokuwa kapewa ili abakie Simba, huku Uongozi wa yanga ukiendelea kumbembeleza hadi leo Chama aende akasaini mkataba kamili ila amegoma hataki na ndio maana hadi sasa chama hajabadilisha Profile yake ya utambulisho kama mchezaji wa simba kwenye page yake ya Instagram.

Huenda Jambo hili likawa kama sakata la MORISON likafika TFF, ngoja tusubiri tuone Dunia ya soka ina mambo sana.

SOMA NA HII  RAJA CASABLANCA IPO SIMBA..FADLU DAVIDS KOCHA MPYA ANAYETAMBA NA MIFUMO HII