Home Habari za Yanga Leo ALI KAMWE AJIBU CHAMA KUTAMBULISHWA BILA JEZI…MASHABIKI WAJA NA KEKI

ALI KAMWE AJIBU CHAMA KUTAMBULISHWA BILA JEZI…MASHABIKI WAJA NA KEKI

Ali kamwe, HABARI ZA YANGA

AFISA Habari wa Yanga Ali Kamwe amezungumzia namna walivyomtambulisha aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama, baada ya kukamilisha usajili huo waliokuwa wanautamani kwa muda mrefu.

Chama alitambulishwa asubuhi ya Julai 1, akiwa anasaini mkataba na Yanga tena bila hata ya kuvaa jezi ya klabu hiyo, hali hii iliibua sintofahamu na maswali mengi kwa mashabiki, wengi wao wakihoji imekuaje mchezaji mkubwa kama huyo ametambulishwa kwa staili hiyo.

Ali Kamwe wakati akizungumza na wanahabari alisema kwamba walifanya hivyo kwa lengo la kibiashara.

“Kuna mjadala nimeusikia eti Yanga kwanini wamemtambulisha mchezaji Mkubwa Chama bila jezi kwanza niwapongeze mmekiri kua ni mchezaji mkubwa pia mbona Mbape ametambulishwa lakini hakuna Jezi Rasmi Mbape kavaa mbona hamsemi” Ally Kamwe – Afisa habari wa Yanga akizungumza na wanahabari.

“Wengi wanauliza mpaka sasa tumenufaika vipi na utambulisho wa Chama. Mpaka sasa tumepokea taarifa za mashabiki wa upande wa pili ambao wamehamia Yanga akiwemo Baba Kamwe nae amemfuata Chama. Wote waliohama tunawaandalia siku maalumu ya kuwapokea”

“Suala la Usajili wa Chama ni sehemu ya biashara yetu. Kila mtu anakiri kuwa usajili wa Chama ni usajili mkubwa. Najua wengi wanauliza kwanini hatujamtambulisha Chama na jezi ya Yanga. Mtiririko wa matukio ya usajili huu wa Chama kwetu ni fursa. Najua wengi wanatamani kujua Chama ataonekanaje na jezi ya Yanga. Hapo ndipo tunalenga kuuza usajili huu” amesema Ally Kamwe

Chama ni miongoni mwa wachezaji wa Kimataifa waliosajiliwa kwa pesa ndefu na watakuwa wanavuta mkwanja mrefu kwa mwezi, amesajiliwa na Yanga kwa dau la Milioni 830 TZS, na atakuwa analipwa mshahara wa Tsh Milioni 35 kwa mwezi.

Mashabiki wa Yanga kuoneshwa kufurahishwa na usajili huo wameamua kumuandalia Keki maalum kama ishara ya kumkaribisha klabuni kwao.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...SHEIKH MNGAZIJA AFICHUA HAYA KUHUSU AFYA ZA WACHEZAJI YANGA...