Home Habari za Simba Leo SIMBA YACHUKUA MWINGINE IVORY COAST…CHAMOU KARABOUE…PIA YATAMBULISHA TEKA LA MAGOLI

SIMBA YACHUKUA MWINGINE IVORY COAST…CHAMOU KARABOUE…PIA YATAMBULISHA TEKA LA MAGOLI

Chamou Karaboue

KLABU YA SIMBA Simba wamefikia makubaliano na Racing Club Abidjan ya Ivory Coast kwa ajili ya kupata huduma ya beki wa kati, Chamou Karaboue, 24, huku Ahoua Jean Charles akitajwa kuwa nyuma ya dili hilo.

Kwa mujibu wa taarifa inaelezwa Chamou Karaboue amekubali ofa ya kusaini Simba mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mmoja.

Muda wowote atatua nchini kwa ajili ya kuungana na Jean Ahoua ambaye msimu uliopita aliibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu Ivory Coast (MVP) huku akifunga mabao 12 na ametoa asisti tisa.

Chamou Karaboue amechaguliwa Kama mbadala sahihi wa Henock Inonga ambae ameuzwa FC Rabat ya Morocco.

Beki huyu mwenye umri wa miaka 24 anatajwa Kama beki bora wa ligi kuu ya Ivory coast iliyomalizika hivi karibuni .

Klabu ya Simba imeendelea kujiimarisha baada ya kutangaza sajili za wachezaji mbalimbali, huku muda huu wakimtambulisha Valentine Mashaka.

Simba Imemtambulisha Valentine Mashaka (18) aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Geita Gold inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC.

Valentino Mashaka msimu uliopita alifanikiwa kuhusika kwenye mabao 7 ya Geta Gold, akifunga mabao 6 na kutoa pasi 1 ya goli, mafanikio mengine aliwahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo mara mbili.

Mashaka amewahi kupita katika klabu ya Ruvu Shooting iliyoshuka daraja. Huu ni moja ya usajili wa kizawa ambao unaweza kuwa ni project nzuri ya Simba kwa misimu ijayo, umri wake ni mdogo na ana kiwango kikubwa.

SOMA NA HII  MASHABIKI WACHOMA MOTO UWANJA...LIGI YA MABINGWA AFRIKA...ISHU NZIMA HII HAPA