Home Habari za Simba Leo JEAN AHOUA KUPEWA JEZI NAMBA 17…TAKWIMU ZAKE ZIKO HIVI.

JEAN AHOUA KUPEWA JEZI NAMBA 17…TAKWIMU ZAKE ZIKO HIVI.

Habari za simba, Jean Ahoua

KLABU ya Simba imefikia makubaliano ya kumsajili aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Stella Adjame ya Ivory Coast, Jean Charles Ahoua kwa kandarasi ya miaka miwili.

Nyota huyo raia wa Ivory Coast ametambulishwa ndani ya kikosi hicho ukiwa ni muda mfupi tu tangu aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Mzambia Clatous Chama kujiunga na Yanga baada ya mkataba wake kuisha huku kukiwa hakuna mazungumzo mapya.

Ahoua ndiye anayetazamwa kama mrithi wa Chama baada ya msimu uliopita kuibuka mchezaji bora (MVP), wa Ligi Kuu ya Ivory Coast alikofunga mabao 12 na asisti tisa na kuwavutia mabosi wa Msimbazi walioinasa saini yake.

Simba imefanikiwa kuinasa saini ya MVP huyo kwa dau kubwa la pesa ambalo linafika Tsh Milioni 600, huku mshahara wake ukikadiriwa kuwa Tsh Milioni 16.

Ahoua ameichagua Simba na kuiakacha Esparance de Tunis ambao pia walikuwa wanamuhitaji, lakini kibunda cha MO Dewji kilikuwa kikubwa kiasi kwamba kilimfanya mchezaji huyo akubali kukipiga Simba.

Sababu nyingine inaelezwa ni mazingira ya hapa Tanzania na aina ya Ligi, kuna wachezaji wenzake kadhaa wa Ivory Coast wanaishi vizuri, Pacome, Aziz Ki, Yao Attouhulla Kwasi, Aubin Kramo, na Ahoua anataka kutengenezea jina lake akiwa Tanzania tena na Simba.

Usajili huo unakuwa wa nne katika timu hiyo baada ya kuwatambulisha beki wa kati, Lameck Lawi aliyetokea Coastal Union, winga Mzambia Joshua Mutale (Power Dynamos) na mshambuliaji Mganda Steven Dese Mukwala aliyetoka Asante Kotoko ya Ghana.

Upande wa mastaa waliotemwa hadi sasa ni aliyekuwa nahodha wa timu hiyo John Bocco, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, Shaaban Idd Chilunda, Luis Miquissone, Kennedy Juma na Henock Inonga aliyetua FAR Rabat ya Morocco huku Chama akijiunga na Yanga.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO ...AHMED ALLY AFUNGUKA NAMUNGO WALIVYOWAPA 'SAPOTI' YA UBINGWA...