Home Habari za Simba Leo BREAKING NEWS…SIMBA YAMTAMBULISHA STRIKA WA MAGOLI…REKODI ZAKE USIPIME

BREAKING NEWS…SIMBA YAMTAMBULISHA STRIKA WA MAGOLI…REKODI ZAKE USIPIME

steve mukwala, habari za simba

NI RASMI Klabu ya Simba Imemtambulisha mshambuliaji Steve Mukwala Dese, Raia wa Uganda kwa mkataba wa miaka mitatu, akitokea klabu ya Asante Kotoko ya Ghana.

Usajili huo umewafanya Simba kutumia zaidi ya Sh Milioni 343 na mshahara wa dola 9000 sawa na Tsh Milioni 25, kupata saini ya straika Mukwala (24) ambaye alikuwa akiwaniwa na vilabu mbalimbali ikiwemo FC Petrocub Hincesti ya Moldova.

Straika huyo anasifika zaidi kwa kutumia mguu wa kulia na uwezo mkubwa wa kufunga kwa kichwa, huku kasi na mabavu zikiwa sifa zake za ziada.

Msimu uliopita aliibuka mfungaji bora namba mbili wa Ligi Kuu ya Ghana kwa kufunga mabao 14 na Assists 5.

Simba itaendelea kutambulisha wachezaji wake wapya, ambapo hadi sasa wametambulisha wawili Joshua Muale na Mukwala.

Soka la Bongo tunaelewa kwamba, Klabu hiyo imekamilisha sajili za wachezaji baadhi akiwemo Elie Mpanzu, Augustine Okejepha, na Valentino Nouma.

Huku wachezaji wengine wakihusishwa zaidi kujiunga na Simba, wanatoka sehemu nyingi, akiwemo Arthur Bada kutoka Asec Mimosas.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema uongozi uko kwenye majadiliano ya kusitisha mikataba ya baadhi ya wachezaji.

Wachezaji wa Simba wanatakiwa kuanza kuripoti Dar kuanzia Julai 1, ili kufanya mazungumzo kabla ya timu hiyo kwenda kuanza maandalizi ya msimu huko Misri.

Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally akizungumzia usajili wa timu hiyo amesema kwamba, usajili wao umekamilika kwa asilimia 97%.

“Usajili wetu umekamilika kwa 97%, hivyo muda wowote tunaanza kutambulisha vyuma vipya, kuna huyo mchezaji tumemsajili ni mrefu zaidi ya goli, haruki anafunga tu”

“Kuna mchezaji mwingine anatoka DR Congo, na kuna huyo mmoja anakimbia kama treni mpya SGR” Alisema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  LEONEL ATEBA AANZA KUWATESA MAKIPA...MANULA BADO YUMO AISEEH