Home Habari za Simba Leo LEONEL ATEBA AANZA KUWATESA MAKIPA…MANULA BADO YUMO AISEEH

LEONEL ATEBA AANZA KUWATESA MAKIPA…MANULA BADO YUMO AISEEH

HAABRI ZA SIMBA-ATEBA

WENGI Walikuwa wanasubiri kumuona mshambuliaji mpya wa Simba Christian Leonel Ateba aliyesajiliwa dakika za jioni kabisa, kabla ya dirisha kubwa la usajili kufungwa.

Katika dimba la KMC Complex Simba inacheza mcheo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Al Hilal ya Sudan, ambapo Leonel Ateba aliweza kufungua akauni yake ya mabao katika timu yake mpya ya Simba.

Wakati ambao Al Hilal wakijiandaa kutengeneza shambulizi kwenda Simba, Debra Fernandes Mavambo alipora mpira katikati  ya uwanja na kuutupa pembeni ya uwanja, ambapo Kijana Kinda aliyeokea Mtibwa Sugar Ladack Chasambi alifanikiwa kuweka kwenye nafasi na kupiga krosi kwenye eneo la hatari la Al Hilal.

Mpira huo ulimkuta Leonel Ateba akiwa kwenye eneo zuri na kuutia kimiani ule mpira.

Lakini dakika chache baadae Aish Manula alionesha uwezo wake baada ya kuka nje kwa muda mrefu sana, ambapo aliokoa mchomo wa hatari sana kutoka kwa Al Hilal,  alitumia mkono wake wa kulia kuokoa krosi iliyopigwa kwenye eneo la hatari.

Kisha baadae Shomari Kapombe aliondoa mpira wa hatari lakini wakaunasa tena Al Hilal kisha ikapigwa krosi nzuri.

Ka mara nyingine tena Manula aliokoa kwa kutumia mkono wake wa Kushoto na mashabiki wa Simba wakakaanga chips majukwaani kwa shangwe na vifijo vya kumshangilia mlinda mlango wao wa muda mrefu.

Hadi kipindi cha kwanza kinatamatika Simba ilikuwa inaongoza kwa bao 1.

SOMA NA HII  AHMED ALLY ASHINDWA KUVUMILIA AITETEA SARE YA SIMBA,AFUNGUKA HAYA