Home Habari za Simba Leo DAU WALILOTUMIA SIMBA KUMNASA STEVE MUKWALA.

DAU WALILOTUMIA SIMBA KUMNASA STEVE MUKWALA.

HABARI ZA SIMBA

Klabu ya Simba imetumia zaidi ya Sh300 milioni kupata saini ya straika Mganda, Steven Dese Mukwala (24) ambaye alikuwa akiwaniwa na klabu mbalimbali ikiwemo FC Petrocub Hincesti ya Moldova.

Straika huyo anasifika zaidi kwa kutumia mguu wa kulia na uwezo mkubwa wa kufunga kwa kichwa, huku kasi na mabavu zikiwa sifa zake za ziada.

Msimu uliopita aliibuka mfungaji bora namba mbili wa Ligi Kuu ya Ghana kwa kufunga mabao 14 na Assists 5.

Muda wowote kuanzia sasa Simba itaanza kutambulisha wachezaji wake wapya, ambapo hadi sasa inaelezwa wamekamilisha sajili za wachezaji baadhi akiwemo Elie Mpanzu, Joshua Mutale, Augustine Okejepha, Steve Mukwala Valentino Nouma.

Huku wachezaji wengine wakihusishwa zaidi kujiunga na Simba, wanatoka sehemu nyingi, akiwemo Kelvin Kapumbu wa Zambia.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema uongozi uko kwenye majadiliano ya kusitisha mikataba ya baadhi ya wachezaji.

Wachezaji wa Simba wanatakiwa kuanza kuripoti Dar kuanzia Julai 1, ili kufanya mazungumzo kabla ya timu hiyo kwenda kuanza maandalizi ya msimu huko Misri.

Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally akizungumzia usajili wa timu hiyo amesema kwamba, usajili wao umekamilika kwa asilimia 97%.

“Usajili wetu umekamilika kwa 97%, hivyo muda wowote tunaanza kutambulisha vyuma vipya, kuna huyo mchezaji tumemsajili ni mrefu zaidi ya goli, haruki anafunga tu”

“Kuna mchezaji mwingine anatoka DR Congo, na kuna huyo mmoja anakimbia kama treni mpya SGR” Alisema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  GAMONDI KUHUSU SIMBA NA YANGA....HAKUNA UNDERDOG