Home Uncategorized NYOTA HAWA WALIZIPA TABU SIMBA NA YANGA, SASA WANAPETA KWENYE TIMU MPYA

NYOTA HAWA WALIZIPA TABU SIMBA NA YANGA, SASA WANAPETA KWENYE TIMU MPYA


 KILA kitu kinatokea kwa sababu ndivyo ambavyo imekuwa kwa wachezaji wengi wa Bongo kupata madili ya kusaini kwenye timu mpya pale ambapo wanaonyesha uwezo wao kwenye mechi ngumu za ushindani.

Rekodi zinaonyesha kwamba asilimia kubwa ya wachezaji ambao wamekuwa wakizitungua Simba na Yanga wamekuwa na kismati cha kupata dili kwenye timu nyingine ama timu hizo zikawapa madili kujiunga nazo.


Leo ikiwa ni Agosti 29, zimebaki siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 31,hawa hapa waliozitungua Simba na Yanga kwenye mechi walizokutana nazo ama kuwapa tabu kimtindo na sasa msimu wa 2020/21 watakuwa kwenye uzi mwingine tofauti na ule wa awali:-


AWESU


Julai 30, Azam FC walimtambulisha kiungo wa Kagera Sugar rasta, Awesu Awesu mwenye jumla ya mabao saba, kwa kandarasi ya miaka miwili.


Kilichompa zali jamaa ni uwezo wake wa kucheza mechi ngumu ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Yanga kwenye Kombe la Shirikisho, Juni 30 aliitungua Yanga bao moja wakati wakipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Mkapa.


Kwenye ligi kati ya mabao 44 yaliyofungwa na timu yake ya zamani yeye alitupia mabao sita ila msimu wa 2020/21 atakipiga ndani ya Azam FC.


MAUYA


Julai 31, Yanga ilimtambulisha kiungo Zawadi Mauya akitokea Kagera Sugar kwa kandarasi ya miaka miwili.


Jamaa hana makuu ila ubabe wake kwa nafasi yake ya kiungo mkabaji ilimpandisha chati. Septemba 26, Uwanja wa Kaitaba wakati Simba ikiibuka na ushindi wa 3-0 alimnyoosha kiungo wa Simba Ibrahim Ajibu kwa mateke zaidi ya matatu.


Jambo hilo liliwafanya wengi kuanza kumfuatilia na uwezo wake ukawavutia Yanga. Kwa tukio hilo alionyeshwa kadi ya njano na alipewa onyo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


WAZIR



Agosti 2, Yanga ilimtambulisha, Wazir Junior kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea Mbao FC, ametupia jumla ya mabao 15 na pasi tatu msimu uliopita, akiwa na mabao mawili kwenye mchezo wa playoffs.


Aliitungua Simba mabao mawili kwenye ligi, alianza Uwanja wa Kirumba, Januari 16 wakati Mbao ikilala kwa mabao 2-1, akamaliza kazi Dar, Uwanja wa Mkapa Julai 16 wakati Simba ikinyooshwa mabao 3-2.

SOMA NA HII  VANDENBROECK KUTUMIA JEMBE JINGINE LA KAZI KWA MBEYA CITY


Yupo zake Yanga sasa licha ya timu yake ya zamani kushuka daraja anaamini kwamba itatusua na kurejea ndani ya ligi msimu ujao.


ILANFYA


Charles Ilanfya kutoka KMC, Agosti 3 tayari alikuwa ameshamalizana na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili. Alitambulishwa rasmi Agosti 14.


Juni 7, Uwanja wa Uhuru wakati Yanga ikikubali kichapo cha mabao 3-0, Ilanfya aliwatungua Yanga bao moja. Moto wake haukuzima, Juni 8 mbele ya Simba, Uwanja wa Mo Simba Arena wakati Simba ikishinda mabao 3-1, Ilanfya alimtungua Aishi Manula bao moja, zilikuwa ni mechi za kirafiki.


Uwezo wake wa kuwatungua Simba na Yanga ukampa dili kijana sasa ni mali ya Simba akiwa amefunga jumla ya mabao sita kwenye ligi alipokuwa KMC.


MORRISON


Balaa lake lipo kwenye namba nane. Agosti 8, Bernard Morrison alitambulishwa ndani ya Simba kwa dili la miaka miwili akitokea Yanga, alifunga mabao manne na pasi tatu ndani ya ligi akiwa ametupia bao moja ndani ya Shirikisho.


Machi 8 aliwatungua Simba Uwanja wa Mkapa mchezo wa ligi kwa mpira wa adhabu nje ya 18. Alitambulishwa ndani ya Simba Agosti 8, saa nane mchana.


Uwezo wake uliwavutia Simba hasa ishu yake ya kupanda mpira na ameshaanza mazoezi na wachezaji wa Simba, huko nako amekuwa akipanda mpira.


SABILO


Agosti 15, Sixtus Sabilo alitambulishwa Namungo FC akiwa huru kwa dili la mwaka mmoja, alifunga mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara.


Ana zali la kuwatungua Simba, Uwanja wa Mkapa ilikuwa Februari 5 wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1.


Sabilo aliingia pia anga za Yanga ila dili lake halikujibu, kwa sasa ameibukia ndani ya Klabu ya Namungo FC inayonolewa na Hitimana Thiery.


SADAT


Agosti 12, Sadat Mohamed alitambulishwa ndani ya Klabu ya Kagera Sugar akitokea Klabu ya Ruvu Shooting.


Moto wake ulikuwa ni balaa kwenye mchezo wa kwanza ndani ya msimu wa 2019/20, Yanga ilikubali kichapo cha bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.


Ilikuwa ni Agosti 28, Ruvu ilisepa na pointi tatu mazima huku mtupiaji wa bao hilo akiwa ni Sadat, atakuwa na jezi ya Kagera Sugar kwa msimu wa 2020/21.