Home Uncategorized MAJEMBE MAPYA POLISI TANZANIA YAWEKA REKODI YA KIBABE VPL

MAJEMBE MAPYA POLISI TANZANIA YAWEKA REKODI YA KIBABE VPL

 RASHID Juma, nyota wa Polisi Tanzania ambaye yupo hapo kwa mkopo akitokea Klabu ya Simba ameweka rekodi ya kibabe ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kufunga bao pekee la umbali mrefu karibia na eneo la 18 akiungana na nyota mwenzake Daruesh Saliboko.

Juma alifanya maajabu hayo kwenye mchezo wao wa ligi uliowakutanisha mbele ya Namungo, Uwanja wa Majaliwa ambapo alipachika bao hilo kwa guu lake la kulia kwa pasi ya Tariq Seif dakika ya 75.

Saliboko naye alifungua akaunti yake ya mabao kwa msimu wa 2020/21 akiwa ndani ya kikosi hicho kwa kufunga bao Septemba 18 mbele ya JKT Tanzania kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

Nyota huyo aliyeibukia Polisi Tanzania akitokea Klabu ya Lipuli alipachika bao hilo kwa mpira wa adhabu uliotengwa nje kidogo ya 18 kwa guu lake la kulia na kuifanya Polisi Tanzania kuwa na jumla ya mabao mawili kibindoni na yote yamefungwa nje ya 18.

Juma ameliambia Spoti Xtra kuwa ni furaha kwake kufunga bao lake la kwanza ndani ya timu mpya huku Saliboko akisema kuwa kazi ndo kwanza inaanza.

SOMA NA HII  VIDEO:MRUNDI ANAYEKIPA SIMBA QUEENS ATAJA AMBACHO ANGEKIFANYA NJE YA SOKA