Home Habari za Yanga Leo ALI KAMWE AWAPIGA DONGO SIMBA…USAJILI WA JOSHUA MUTALE

ALI KAMWE AWAPIGA DONGO SIMBA…USAJILI WA JOSHUA MUTALE

Habari za Yanga, Ali Kamwe.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga SC, Ally Kamwe amesema kuwa usajili wanaoufanya watani zao wa jadi, Simba SC ni wa kawaida hivyo wategemee mateso tena msimu ujao.

Simba wametambulisha wachezaji watatu ambao ni Joshua Mutale kutoka Power Dynamos ya Zambia, Lameck Lawi kutoka Coastal Union ya Tanga na Steven Mukwala raia wa Uganda akitokea Asante Kotoko ya Ghana.

Mukwala msimu uliopita alikuwa alikuwa mfungaji namba mbili wa Ligi Kuu yaGhana, akiwa na magoli 14, na asisti 5.

“Kosa kubwa mnalofanya ni kulinganisha sajili za yanga na wachezaji wengine, mnawapa presha wachezaji wadogo wadogo. Chama yupo kwenye top 20 ya wachezaji bora wa muda wote wa CAF. Huyu Joshua wa Simba sio mchezaji mbaya ila ni aina ya wachezaji ambao tulikuwa nao miaka mine iloiyopita.

“Sidney Urikob, Patrick Sibomana, Juma balinya ni aina ya wachezaji ambao tulikuwa nao miaka mine iliyopita. Zambia ina mwamba mmoja tu, pamoja na straika kennedy Musonda wachezaji wengine ni wa shirikisho ambao ukienda nao hatua ya awali mtawasha moto uwanjani mtafukuzwa.

“Sisi tumetambulisha mtu mmoja tu nchi nzima imetetemeka kwa sababu huyo mtu ni mwamba,” alisema Ali Kamwe.

Alichokisema Ali Kamwe linafikirisha kidogo ambapo shabiki mmoja huko mitandaoni alimjibu kwa kumuuliza swali, Chama alikuwa Simba misimi 6 nyuma,  Je na wao  Simba wasemaje kwenye usajili huo wa Yanga?

SOMA NA HII  TETESI ZA USAJILI: MESSI KUNG'OLEWA PSG...WAARABU WAMPA MIL 1 KILA DK 1...POGBA ACHEZA DK 35 MSIMU MZIMA