Home Habari za Simba Leo NI MARUFUKU KUVAA JEZI ZA YANGA…MANGUNGU NA MO DEWJI WAWEKA KIPINGAMIZI

NI MARUFUKU KUVAA JEZI ZA YANGA…MANGUNGU NA MO DEWJI WAWEKA KIPINGAMIZI

HABARI ZA SIMBA

KABLA YA Kusafiri kwenda Misri kwaajili ya Manadalizi ya Msimu mpya, Simba ilijifungia kwenye hoteli moja eneo la Mbezi Beach na kufanya kikao kizito.

Katika kikao wachezaji waliambiwa ni marufuku kuvaa nguo ambazo hazitakiwi kuzivaa wakiwa Simba na kwamba nguo yoyote inayoashiria rangi ya jezi zinazotumiwa na watani wao ni marufuku kuvaliwa kambini au nje ya kambi.

Nguo rasmi za kuvaa wakati wakiwa kambini ni zenye nembo ya wadhamini na ile ya klabu, hivyo atakayekutwa amekiuka utaratibu atajiingiza matatizoni.

“Hatutakiwi hata kuvaa jezi za Yanga tukibadilishana na wenzetu wa kule na kama ukitokea umebadilishana na mwenzako, unatakiwa kuishika na kwenda kuitunza ndani kwako na sio kuivaa pale uwanjani. Lazima kila mchezaji azilinde nembo za klabu pamoja na wadhamini,”

Uongozi wa Klabu hiyo ulifanya kikao hicho cha pamoja ikiwahusisha Muwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Mohammed Dewji, Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu, Wajumbe wa bodi ya Simba kwa ujumla, benchi la ufundi na wachezaji.

Lengo lilikuwa ni kupeana utaratibu mpya, malengo ya klabu na kjiandaa kwa msimu mpya, ikiwemo kufahamiana kwa wachezaji wapya na wa zamani, benchi jipya la ufundi na Viongozi.

Itakumbukwa hivi karibuni kumekuwa na taarifa za wachezaj wa timu hiyo kuhujumu hali iliyokuwa inapelekea matokeo mabaya ndani ya uwanja.

Kauli ya hujuma kwa wachezaji ilitolewa na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah Try Again, alipokuwa akitangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

“Kuna Taarifa za baadhi ya wachezaji wetu kuihujumu timu, hilo tumelifahamu na ripoti kamili nimemtumia Muwekezaji MO Dewji ataifanyia kazi”

Hadi sasa Simba imeachana na wachezaji wakubwa kadhaa ikiwemo Clatous Chama ambaye mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya hayakufanikiwa, na akajiunga na Ynaga, Saidoo Ntibazonkiza, Henock Inonga aliyeuzwa, Luis Miquissone John Bocco na Kennedy Juma.

Huku majina mengine kama Babacar SAR, Sadio Kanoute, Par Omar Jobe, Willy Esomba Onana, Aubin Kramo yakiwekwa kwenye mabano muda wowote yatatanazwa kuachwa.

SOMA NA HII  YANGA NA SIMBA... ZIMETUHAKIKISHIA KUPELEKA TIMU 4 KIMATAIFA MSIMU UJAO