Home Habari za Yanga Leo NUNGUNUNGU ALIWA KICHWA JANGWANI…KAMWE AFUNGUKA

NUNGUNUNGU ALIWA KICHWA JANGWANI…KAMWE AFUNGUKA

Habari za Yanga- Jonas Mkude

Taarifa zinaeleza kua kiungo wa zamani wa klabu ya Simba Jonas Mkude “Nungunungu” huenda akapewa mkono wa kwaheri ndani ya klabu ya Yanga baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya timu hiyo.

Kiungo Mkude alipewa mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu ya Yanga na umemalizika huku klabu hiyo ikielezwa haina mpango wa kumuongeza kandarasi mpya, Hivo jambo lililobaki ni moja tu kupewa mkono wa kwaheri ndani ya viunga vya Jangwani.

Jonas Mkude aliyejiunga na Yanga akitokea klabu ya Simba amekua hana msimu bora sana ndani ya kikosi hicho, Kwani amekua hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara hivo klabu hiyo inaelezwa kufikia uamuzi wa kuachana nae.

Mkude atakumbukwa zaidi mitaa ya Jangwani kupitia mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns, Ambapo alionesha kiwango bora sana katika michezo yote miwili kuanzia mchezo wa kwanza hapa Tanzania na mchezo marudiano kule Afrika Kusini.

Lakini upande wa Pili wa klabu hiyo umeendela kufurahia usajili mkubwa uliofanywa na Uongozi wao.

Ali Kamwe, Afisa Habari wa Yanga amebainisha kuwa haikuwa kazi rahisi kuwapata wachezaji wenye uwezo mkubwa hilo lipo wazi na linaongeza thamani ya ligi ya Tanzania.

“Msimu huu hata msiposema mawe yatazungumza kwamba Yanga tuna timu bora kwa kuwa kuna wachezaji wazuri wenye ubora na hilo linafanyika kwa sasa kuwa imara kila eneo ndani ya uwanja.

“Kila Mwanayanga anafurahi kwa sasa kwa sababu kila eneo kuna wachezaji bora na wenye uwezo mkubwa hili linatupa nguvu ya kuwa imara kwenye mashindano ambayo tutashiriki.”.

Usajili wa kwanza ndani ya Yanga ambao umeleta mtikisiko Bongo ni wa Clatous Chama ambaye ameibuka hapo bure akitokea Simba yeye ni kiungo mshambuliaji.

Saini ya Stephene Aziz Ki ambaye alitambulishwa Julai 10 kuwa bado ni Mwananchi ilizua gumzo barani Afrika kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za timu mbalimbali.

SOMA NA HII  KUMBUKIZI HIZI ZA DABI YA WATANI WA JADI...ZAIBEBA SIMBA WAZI WAZI