Home Habari za Simba Leo SIMBA INASUKA KIKOSI CHAKE…KAZI IMEANZA

SIMBA INASUKA KIKOSI CHAKE…KAZI IMEANZA

Habari za Simba- Fadlu Davids

MTAALAMU KABISA Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba ana kibarua cha kusuka upya kikosi hicho kuelekea msimu wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani kitaifa na kimataifa.

Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika itasubiri mshindi wa mchezo kati ya Uhamisho dhidi ya Libya kwa kuwa haitaanzia hatua ya awali.

Mbali na Simba kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Coastal Union pia ipo anga la kimataifa baada ya kugotea nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Ahmed Ally, Menejawa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema: “Kocha Fadlu anatambua kitu ambacho Wanasimba wanahitaji hivyo anasuka kikosi kazi kwa ajili ya kuleta ushindani akishirikiana na benchi zima la ufundi.

“Wachezaji wapo tayari wanaendelea na mazoezi na wapo wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi kwa msimu wa 2023/24 tunaamini kwamba tutafanya vizuri mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”

Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni Mzamiru Yassin, Ayoub Lakred, Ally Salim, Hussen Abel, Hussen Kazi, Che Malone Shomari Kapombe huku Aishi Manula akibaki Bongo akitajwa kuwa huenda akaibukia Azam FC.

Simba katika dirisha hili la usajili ambalo linaendelea, imesajili mshambuliaji Steven Mukwala ambaye ametoka Asante Kotoko ya Ghana, beki Valentin Nouma akitokea timu ya St. Eloi Lupopo ya DR Congo.

Beki ya kati wamemuongeza Chamou Karaboue na Abdulrazack Mohamed Hamza (23) akitokea klabu ya Supersport United ya Afrika Kusini.

Kwenye eneo la kiungo imemsajili Joshua Mutale, Augustine Okajepha, Debora Mavambo, Jean Charles Ahoua na Yusuf Kagoma hivyo ni wazi imejipanga kutengeneza timu bora kwenye maeneo yote ya uwanja.

Iko wazi Simba hadi sasa imeachana na wachezaji kadhaa akiwemo John Bocco aliyetambulishwa JKT Tanzania, Saidoo Ntibazonkiza, Clatous Chama aliyejiunga na Yanga, Kennedy Juma, Sadio Kanoute anayehusishwa kujiunga na JS Kabyile ya Algeria inayonolewa na Bnechika.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO....AHMED ALLY ATAMBA SIMBA KUFANYA USAJILI WA KUTIKISA AFRIKA...VYUMA VIPYA HIVI HAPA...