Home Habari za Yanga Leo YANGA YANASA BEKI MKENYA…YATANGAZA VITA KWA WATANI ZAO SIMBA

YANGA YANASA BEKI MKENYA…YATANGAZA VITA KWA WATANI ZAO SIMBA

Habari za Yanga Leo

KLABU YA YANGA inaendelea kushusha vyuma na safari hii imetua kwa beki wa kati raia wa Kenya, Anitha Adongo kwa ajili ya msimu ujao.

Hadi sasa Yanga Princess inayoshiriki Ligi ya Wanawake (WPL) inahusishwa kumalizana na wachezaji wanne wa kigeni akiwemo Danai Bhobho kutoka kwa watani zao, Simba Queens.

Kwa mujibu wa Mwanaspoti wanasema kwamba, Rafiki wa karibu wa mchezaji huyo wa zamani wa Alliance Girls ya Mwanza alisema ni kweli Yanga ilimtafuta na kufanya mazungumzo naye kilichobani ni kusaini tu.

“Kwa sasa yupo Kenya kwenye mapumziko na Yanga walimtumia mkataba ausome na wakaelewana ingawa kulikuwa na ofa pia kutoka Fountain lakini mwenyewe hajaridhia huko kutokana na changamoto ya klbu hiyo,” alisema rafki wa mchezaji huyo na kuongeza

“Wanasubiri tu utaratibu kutoka kwa Yanga baada ya kuwarudishia majibu ya kuwa ameridhia kujiunga nao, atakuja kwenye tamasha la Yanga Day ndio atasaini mkataba.”

Anita msimu uliopita alikuwa nahodha wa Alliance Girls akiisaidia timu hiyo kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

Yanga Princess haikuwa na msimu mzuri kwenye Ligi Kuu ya Wanawake, kwani haikuweza kutwaa ubingwa wa Ligi hiyo huku pia baadhi ya wachezaji wake muhimu wakichukuliwa na Mnyama Simba.

Itakumbukwa kwamba Rais wa klabu hiyo Injinia Hersia wakati akizungumiza usajili wa jumla kwa timu ya wanaume na wanawake, alisema kwamba anaelewa kuwa timu yao ya wanawake haifanyi vizuri hivyo amejipangga kufanya usajili mzuri ili kuweka heshima na kwenye soka la wanawake.

Injinia Hersi aliyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye Mkutano Mkuu wa Yanga mwaka 2024.

SOMA NA HII  AUCHO AWAGEUKIA WACHEZAJI..."MKITAKA NIWE MTU MBAYA NITAFANYA HIVYO