Home Habari za Simba Leo UTABIRI WA SOKA LA BONGO UMETIMIA…AWESU AVAA JEZI YA SIMBA

UTABIRI WA SOKA LA BONGO UMETIMIA…AWESU AVAA JEZI YA SIMBA

HABARI ZA SIMBA-AWESU

Klabu ya Simba imetambulisha kiungo mshambuliaji Awesu Awesu kutoka KMC kwa mkataba wa miaka miwili.

Awesu amejiunga na Simba akiwa mchezaji huru baada ya kununua mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia na KMC aliyodumu nayo kwa miaka mitatu.

Mbali na KMC, Awesu amewahi kutimikia timu za Kagera Sugar, Azam FC na Mwadui FC kwa nyakati tofauti.

β€œTumefanya marekebisho makubwa ya kikosi kwa kusajili nyota wapya ndio maana tunaongeza na wachezaji wazawa wenye ubora,”

β€œKuelekea msimu mpya wa mashindano tunaandaa kikosi imara ambacho katika kila nafasi kutakuwa na wachezaji wenye ubora unaolingana.” Imeandika taarifa ya Simba.

Soka la Bongo tulitoa taarifa juu ya usajili wa Awesu kwenda Simba tangu Julai 7 mwaka huu, na sehemu ya ripoti yetu ilikuwa hivi.

UONGOZI wa Simba umefanikiwa kunasa saini ya kiungo wa KMC FC, Awesu Awesu kwa mkataba wa miaka miwili baada ya makubaliano ya viongozi wa pande zote mbili.

Imeelezwa kuwa msimu ujao kiungo huyo ataonekana uwanjani akiwa na jezi ya rangi nyekundu na nyeupe kwa msimu wa 2024/25 wa Ligi Kuu Bara na kombe la Shirikisho Afrika.

Usajili ya kiungo huyo ni kufikia mapendekezo ya benchi la ufundi ambalo lilipendekeza kusajili kwa mchezaji mzawa na Awesu ikiwa ni sehemu ya jicho la Wekundu hao wa Msimbazi.

Nyota huyo ambaye amekuwa akisifiwa na Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe alikiri kuwa katika viungo bora Awesu atakuwa kwenye orodha yake na angepewa nafasi ya kupendekeza usajili karata yake angeitupia kwa nyota huyo.

Taarifa zilizopatikana kuwa uongozi wa Simba umefanikiwa kuzungumza na mchezaji huyo na kuwaeleza ana mkataba wa mwaka mmoja na kukaa meza moja na Waajiriwa wake walikubaliana kununua mkataba ulisalia.

β€œNi kweli mazungumzo yalienda vizuri na Awesu ana mkataba wa mwaka mmoja ambao Simba wamekubali kuununua na kiungo huyo kuwa mali yao kwa msimu mpya wa mashindano,” alisema mtoa habari huyo.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO SIMBA WATAKAVYONUFAIKA NA MABILIONI YA M-BET...KILA MWAKA DAU LITAONGEZEKA MARA DUFU...