Home Habari za Simba Leo MZAMIRU HAWANA PRESHA SIMBA…VIUNGO 8 NA WALA HAWAZI

MZAMIRU HAWANA PRESHA SIMBA…VIUNGO 8 NA WALA HAWAZI

Habari za Simba leo

KIUNGO wa Kazi Chafu Mzamiru Yassin amesema hana presha yoyote ndani ya Simba licha ya kusajiliwa mashine kadhaa mpya zinzocheza eneo lake, kwa vile anaamini kila mchezaji wa kikosi hicho kinachoendelea kujifua jiji la Ismailia, Misri ana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

Simba imeongeza mashine kadhaa mpya katika eneo hilo baada ya kuondoka kwa Sadio Kanoute na Babacar Sarr waliotumua JS Kabylie ya Algeria, wakiwamo Yusuf Kagoma, Augustine Okajepha, Debora Mavambo na Awesu Awesu wanaoungaa na Mzamiru na Fabrice Ngoma waliosalia kutoka msimu ulioopita.

Mzamiru alisema maandalizi ya msimu mpya kukiwa na benchi la ufundi jipya hakuna hofu kwa mchezaji yeyote zaidi ni kupambana kuonyesha nini kimekufanya uwe ndani ya kikosi.

“Ni kweli kuna sajili nyingi lakini sina sababu ya kuwa na hofu naamini nina kila sababu ya kucheza kikosi cha kwanza kutokana na uzoefu nilionao pamoja na kufahamu nini Simba inataka kwa wakati upi,” alisema nyota huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar anayeitumikia pia Taifa Stars, aliyeongeza;

“Wachezaji wote tuna nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kilichopo ni ushawishi kwenye uwanja wa mazoezi na kipindi hiki ambacho mwalimu ni mpya kila mmoja anapambana kuonyesha uwezo wake ili kumshawishi.”

Mzamiru alisema Simba wanatambua mchango wake kikosioni na ndio maana wamemuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo na anawaahidi wanasimba kufanya mambo mazuri ili kuipambania timu hiyo iweze kufikia mafanikio.

Akizungumzia michuano ya kimataifa na Simba ikiiwakilisha Tanzania Kombe la Shirikisho Afrika, Mzamiru alisema baada ya kufanya vizuri Ligi ya Mabingwa kwa kucheza hatua ya robo fainali mara tatu mfululizo anatamani kuona wanacheza fainali Shirikisho Afrika kama iliyofanywa na Yanga misimu miwili iliyopita.

“Maandalizi mazuri na utayari wa wachezaji nafikiri ndio siri kubwa ya kufikia mafanikio Kimataifa matarajio yangu ni kuona timu yangu inacheza hatua ya fainali na hatimaye kutwaa taji la kombe la Shirikisho hilo linawezekana, endapo benchi la ufundi, wachezaji na uongozi kwa ujumla tutawekeza misingi imara na bora kupitia kambi ya maandalizi.”

Simba imepangwa kuanzia raundi ya pili ya michuano hiyo ambayo mwaka 2022 ilifika robo fainali mara ilipotemwa kutoka Ligi ya Mabingwa kwa kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, ikisubiri mshindi kati ya Uhamiaji ya Zanzibar na timu wawakilishi kutola Libya ambayo bado haijafahamika.

Wawakilishi wengine wa nchi Yanga, Azam na JKU zenyewe zinaanzia raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Coastal Union iliyorejea katika michuano ya Sgirikisho tangu mwaka 1989 itaanzapia pia raundi ya kwanza kama Uhamiaji.

SOMA NA HII  𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐋𝐀 𝐎𝐍𝐀𝐍𝐀 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐐𝐀𝐓𝐀𝐑 𝐋𝐈𝐌𝐄𝐅𝐄𝐋𝐈 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈