Home Habari za michezo SIMBA YAWAONGEZA MKATABA MZAMIRU & ISRAH…MWINGINE ATAMBULISHWA

SIMBA YAWAONGEZA MKATABA MZAMIRU & ISRAH…MWINGINE ATAMBULISHWA

HABARI ZA SIMBA

KIUNGO wa Simba fahari ya Morogoro, mtaalamu kabisa wa dimba la kati Mzamiru Yassin Selemba, ameongeza mkataba wa kusalia Simba hadi mwaka 2026.

Mzamiru ameongezewa mkataba wa miaka miwili baada ya kuwepo taarifa za mchezaji huyo kuachwa Simba, na atajiunga na timu ya Singida Black Star.

Kupitia taarifa rasmi ya klabu ya Simba, imeandika kwamba Mzamiru Yassin ameongeza miaka miwili.

“Kiungo mkabaji Mzamiru Yassin amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia katika kikosi”

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alijiunga na Simba mwaka 2016 akitokea Mtibwa Sugar, kwahiyo amehudumu klabuni hapo kwa miaka 8.

Katika vipindi vyote akiwa Simba Mzamiru amekuwa akiongezeka kiwango siku hadi siku, na chini ya Juma Mgunda kiwango chake kimeimarika zaidi.

Kocha Mgunda aliwahi kuzungumzia kiwango cha mchezaji huyo, alisema kwama Mzamiru ni mchezaji anayetakiwa kupewa majukumu.

“Ujue kwamba Mzamiru sio kwamba ni mchezaji mbaya, na sio kwamba mimi namuwzea sana, bali Mzamiru ni mchezaji ambaye anatakiwa umpe maelekezo maalum anapokuwa uwanjani” Juma Mgunda kuhusu Mzamiru Yassin.

Mbali na Mzamiru Yassin Simba pia imemuongeza mkataba beki wake wa kulia Israel Mwenda hadi mwaka 2026.

Simba inaendelea kuachana na wachezaji wake ambapo hadi sasa imeachana na wachezaji wake watano ikwemo John Bocco, Saidoo Ntibazonkiza, Kennedy Juma, Shabani Idd Chilunda, na Henock Inonga ambaye ameuzwa katika klabu y AS Far Rabat.

SOMA NA HII  FADLU DAVIDS AWAKALISHA CHINI MUTALE NA MUKWALA