Home Habari za Yanga Leo GAMONDI WALA HANA HOFU NA KOSI LAKE.

GAMONDI WALA HANA HOFU NA KOSI LAKE.

GAMONDI AENDELEA KUWABURUZA SIMBA...AWAPIGA PIGO HILI JIPYA...KUBWA KULIKO

YANGA baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki ndani ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya, wala hajaumizwa na matokeo hayo lakini akawapa tano mastaa wa timu hiyo walivyokiwasha kwa madiba.

Yanga ilipoteza kwa mabao 2-1 mbele ya FC Augsburg ya Ujerumani katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mbombela, jijini Mpumalanga ikiwa ni mechi za michuano ya Kombe la Mpumalanga iliyoandaliwa na klabu ya TS Galaxy ya huko.

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi alisema mechi ya juzi ilikuwa ya kuangalia kiwango cha mazoezi ya kikosi hicho tangu wameanza maandalizi ambapo wala hataki kuweka akilini matokeo ya mechi hiyo.

Gamondi alisema licha ya timu kupoteza lakini amefurahishwa na namna wachezaji wake wale wapya na wale waliokuwepo walivyocheza kikubwa mchezo huo.

Kocha huyo raia wa Argentina, alisema mechi hiyo imewaongezea kitu wachezaji lakini kama makocha wamepata majibu ya kipi kinatakiwa kuendelea kufanyiwa kazi.

“Kwangu mimi matokeo hayakuwa kitu muhimu sisemi hivi kwasasabu tumepoteza hata kama tungeshinda ningesema hivi, kuna mambo ambayo tutayazingatia hasa yale ambayo tumekuwa tukijaribu kuyajenga wakati huu tunaandaa timu kwa ajili ya mashindano ya msimu ujao,” alisema Gamondi na kuongeza;

“Tulicheza dhidi ya timu kubwa Ulaya lakini angalia namna wachezaji walivyocheza kikubwa, walikuwa na utulivu mkubwa, wanajiamini na kucheza kwa nidhamu kubwa wakati wa kushambulia na hata kukaba na kwa makocha tumepata majibu ya kipi tunatakiwa kuendelea kukifanyia kazi, wapi tunaridhika lakini kwa wachezaji wetu nao wamejiongezea kitu nadhani kila mtu aliona namna tulivyoonyesha kuwa kuna tofauti ndogo kati ya FC Augsburg na sisi Yanga.”

Yanga itaendelea na maandalizi yao hayo huko Afrika Kusini na keshokutwa Jumatano itacheza mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya wenyeji wao wa TS Galaxy ya hapo Afrika Kusini.

SOMA NA HII  INJINIA HERSI AVUNJA UKIMYA YANGA...USAJILI UKO HIVI...