Home Habari za Simba Leo MNYAMA KUZINDUA SIMBA DAY MIKUMI…KUTUMIA SGR…MAMBO YOTE NI MWAKE

MNYAMA KUZINDUA SIMBA DAY MIKUMI…KUTUMIA SGR…MAMBO YOTE NI MWAKE

Habari za Simba, Ahmed Ally

UKISEMA Tamasha la Simba Day limeanza kuitetemesha Nchi utakuwa sahihi baada ya Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Simba kutoka kona mbalimbali nchini kujiweka tayari kwa mtoko huo.

Simba kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania wanatarajia kuzindua wiki ya Simba ndani ya Morogoro Jumatano ya Julai 24, mwaka  huu kwenye  hifadhi ya Mikumi.

Uzinduzi wa tamasha hilo kilele chake kitafanyika  Agosti 3 mwaka huu, Simba itacheza  mechi ya kirafiki dhidi ya APR ya Rwanda, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Viingilio vya kilele cha Simba Day kushuhudia mchezo huo , Mzunguko ni 5000, Orange 10,000, VIP C, 20,000, B 30,000, A 40,000 na Platinum 200,000 na kuanza kuuzwa rasmi leo.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula, amesema wanalenga kuzindua Wiki ya Simba kuipeleka Morogoro na kitovu chake katika mbuga ya Mikumi.

“Klabu inajali wajibu wake kwenye Serikali tumeamua kutangaza utalii na kukuza uchumi wetu. Hatutaenda moja kwa moja katika hifadhi tutaanzania Morogoro katika matawi halafu tutamalia kwenye hifadhi hizo,” amesema Kajula.

Ameongeza kuwa baada ya uzinduzi ya wiki ya Simba Morogoro,  wataenda katika hifadhi hiyo ambayo ndani yake kuna uwanja wa mpira wa miguu na kucheza mechi ya kirafiki kati ya Simba ambapo msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba atakuwa sehemu ya kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi dhidi ya wazi wa Morogoro.

Naye Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema lengo la ushirikiano wa kuunganisha taasisi tatu ni kuboresha tamasha la Simba ambalo kilele chake itakuwa Agosti3, mwaka huu.

“Wiki ya Simba tunaenda kufanya uzinduzi Morogoro mjini baada ya hapo tutaenda Hifadhi ya Mikumu ya Mikumi, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Simba lakini pia kuhamasisha watanzania na wakigeni kuja kufanya utalii.

Kwa hali hiyo tumeamua kuweambia Watanzania kuwa wanaweza kwenda kufanya utalii wa ndani kwa bei rahisi lakini tunatangaza bidhaa mpya wa SGR (Joshua Mutale),pamoja na kuunga mkono wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan katika mradi huu,” amesema Ahmed.

Amesema Simba wamechukuwa mabehewa matatu, maeili yakiwa ya watu wa burudani akiwemo King Faida na Malaika Bend na behewa la tatu litakuwa na watu wasipenda kelele lakini pia kutokana na maombi ya mashabiki wengi wameongeza behewa la nne.

Ameweka wazi taratibu ya wiki ya Simba, Julai 26, kutakuwa na droo ya makundi kwa ajili ya Julai 27 mwaka huu watakuwa na bonanza la Matawi yote ya Dar es Salaam kutafuta shabiki bora wa msimu litakalofanyika uwanja wa Mwembe Yanga.

“Juali 28 tutaenda Mbagara kwa ajili ya kuhamasisha , kila mwanasimba, tawi wanajikusanya kwa pamoja waende kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji maalum  na watu  kupata baraza zao kwa msimu na kurejesha kwa jamii,” amesema Ahmed.

Mkurugenzi Mkuu  wa Shirikia la Reli Tanzania,, Masanja Kadogosa amesema viongozi wa Simba wamefikiria kitu kizuri kwa sababu wanasapoti juhudi za Rais Samia kuchochea utalii wa ndani.

“Tutaenda Morogoro pamoja na tutarudi pamoja kwa kutumia Treni ya SGR, tutashirikiana na Simba kuhakikisha wanafanikisha jambo lao la kuzindua wiki ya Simba,Tukio la kuzarendo kwa nchini yao  tunaanza kwa hiyo Simba inaweza kusaidia kututambulisha na naamini kwa ushirikiano huo tunatarajia kuona makubwa,” amesema.

SOMA NA HII  SAKATA LA AWESU NA SIMBA LIPO HIVI...KIJANA AGOMA KURUDI