Home Habari za Yanga Leo MBABE WA AL AHLY NDANI YA YANGA…NYIE HAMUOGOPI

MBABE WA AL AHLY NDANI YA YANGA…NYIE HAMUOGOPI

Habari za Yanga SC

MICHUANO YA CAFCL hatua ya makundi Al Ahly Mapharao wa Misri walikuwa ni imara kwenye upande wa ulinzi kutokana na ukuta wao kutoruhusu mabao mengi ya kufungwa katika mechi za ushindani.

Rekodi zinaonyesha kuwa mabingwa hao ambao walimenyana na Simba kwenye hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika walifugwa bao moja pekee katika hatua ya makundi.

Ikumbukwe kwamba mtupiaji alikuwa ni Pacome Zouzoua kwa shuti akiwa nje kidogo ya 18 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Pacome Zouzoua bao lake lilitajwa kuwa bao bora la wiki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika alikuwa anatajwa kuwa miongoni mwa nyota ambao wangekuwa kwenye changamoto mpya msimu wa 2024/25 baada ya kuwatikisa Al Ahly lakini bado yupo ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Kwenye ligi alicheza mechi 21 akitupia mabao 7 na pasi 3 za mabao msimu wa 2023/24 na Yanga ilitwaa taji la ligi safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 71 ikiwa namba moja kwa timu zilizofunga mabao mengi zaidi.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AFICHUA SIRI HII YA KUIBANJUA YANGA...AMEFUNGUKA HAYA