Kitendo cha Klabu ya Simba SC kuificha timu yao iwe kwa makusudi au bahati mbaya ya mazingira kimewasaidia kutengeneza hamu ya mashabiki wake na hata wapinzani wao kutaka kuwaona wanachezaje .
Wachezaji wa Yanga wameoonekana kwenye mechi tatu mfululizo na usajili wao tumeuona lakini Simba ni kama wameficha white dhidi ya black kwenye pooltable kitendo kilichosababisha mashabiki wengi kuwa na shauku ya kuwaona.
Hali hiyo itaendelea kuipa faida Simba hata baada ya Simba day kwa sababu mijadala bado itaendelea kama mashabiki wataridhishwa na kiwango au hata kama hawataridhishwa.