Home Habari za Yanga Leo NI MUDA WA KUTUBU…KAULI TATA ZA WACHAMBUZI KUHUSU YANGA

NI MUDA WA KUTUBU…KAULI TATA ZA WACHAMBUZI KUHUSU YANGA

habari za yanga-NABI

BAADA ya Yanga kufanya mabalaa yake kwenye michezo yake miwili ya Ngao ya Jamii na kutwaa tena taji hilo, wamesababisha kutengeneza stori kubwa mtaani kwa kiwango chao ambacho kinaonekana kuwa tishio kubwa kwa timu za Ligi Kuu.

Yanga kwa sasa ni timu yenye kikosi chenye ubora mkubwa, kina wachezaji wenye majina makubwa ana uwezo mkubwa akiwemo Aziz Ki, Pacome, ChAMA, NA Dube, Maxi Nzengeli na Khaleed Aucho.

Wachambuzi wa michezo kutoka kituo cha habari cha EFM, kwa nyakati tofauti wamejikuta wakitoa kauli zifuatazo ambazo zinaelezea kiwango cha Yanga kwa sasa.

“Unajiuliza ! Kama Azam mwenye quality hii anataabika hivi licha ya kuanza pre-season mapena, sijui zile timu zetu zinazoanza maandalizi 1/8 na usajili umejikita kwa wazawa tu itakuwaje!!! “-Tigana Lukinja-Mchambuzi wa Efm Radio.

“Kwa jinsi nilivyoangalia mechi za ngao ya Jamii nimeanza kupata wasiwasi huenda Yanga wakamaliza ligi UNBEATEN tena. Kama Simba na Azam timu ambazo tunasema zinagombea Ubingwa na Yanga zinapigwa hivi kwa kuzidiwa kila kitu vipi kwa timu kama Ken gold Pamba na wengine ?! “-Wilson Oruma, Mchambuzi wa Efm Radio.

“Yanga sio tu Mabingwa wa Ngao, ila WAMESTAHILI kuwa Mbaingwa. Unapocheza nao inabidi uwe umefanya homework yako vizuri sana, usijaribu jambo lolote jipya ambalo halijawahi kufanyika kwenye timu wachezaji wakalielewa vyema, kumbuka ukicheza nao ndio unapima ubora wako tena kwenye jambo ambalo limezoeleka, vinginevyo ukitia udambwi dambwi wanakuchana chana.”

” Yanga ni timu iliyotimia na yenye ubora katika kila idara kuliko nyingine yoyote nchini kwa sasa, wachezaji na benchi la ufundi wana ubora mkubwa sana. Hongera GONGOWAZI timu ya Hayati Mzee SAID KAZUMARI MTIPA.” -Jemedari Said.

SOMA NA HII  KISA MECHI ZA CAF....ALLY KAMWE AMPA 'MAKAVU LIVE' AHMED ALLY..."ANATUFATA FATA SANA HUYU"...