HABARI ZA SIMBA-ATEBA
Habari za Simba Leo

UJIO WA ATEBA SIMBA…WAWILI ROHO JUU…FREDY NAE MMMH

Abubakar August 16, 2024 4:50 pm

Klabu ya Simba jana imekamilisha usajili wa Leonel Ateba kutoka USM Alger ya Algeria na saa 4:00 usiku ikamtambulisha rasmi.

Wakati Wanasimba wakitamba na ujio wa Ateba, presha imehamia kwa wachezaji wawili ambao mmojawapo ataonyeshwa mlango wa kutokea ili kumpisha Ateba.

Kwa habari za ndani kutoka Simba, zinaeleza kwamba Mshambuliaji wa timu hiyo Fredy Michael Koublani bado ataendelea kusalia Msimbazi.

Badala yake Uongozi wa Simba unafanya jitihada za kuliondoa jina na Mlinda mlango wao Ayoub Lakred kwenye mfumo wa usajili, na kisha watampa muda mwingi wa kupona jeraha lake alilolipata mazoezini.

Simba hawataki kuachana na Lakred kwa sasa akiwa na hali ya majeraha, bado wanaimani na kipa huyo kuwa akipona atarudi kwenye kuipambania Simba.

YANGA YACHIMBA MKWARA MZITO…VIATL’O WAJIANDAE METACHA APAMBANIA TUZO NA MATAMPI