HABARI ZA YANGA-MZIZE
Habari za Yanga Leo

GAMONDI AWEKA NGUMU KWA WYDAD

Abubakar August 21, 2024 5:28 pm

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anafurahishwa na Clement Mzize na anataka nyota huyo asiuzwe kwenda Wydad Casablanca kwa gharama yoyote!

Jaribio la ZAIDI ya Bilioni 1.6 na vipengele vingine rafiki vilivyowasilishwa na Wydad havijapitishwa na Yanga huku viongozi wakimridhia Gamondi ambaye ana imani kubwa kwa Mzize na amekuwa kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu na Kocha huyo.

Wydad wanakusudia kufanya jaribio la mwisho la kumsaini nyota huyo ama kumchukua kwa Mkopo saa chache baada ya kukamilisha uhamisho wa Casius Mailula kwa Mkopo pia kutoka Mamelodi Sundowns.

Katika hatua nyingine klabu hiyo imehakikishiwa kuwa Feisal Salum hatapatikana kwa sasa kutoka Azam FC na IMERIDHIA lakini bado haijakata tamaa suala la beki Yeison Fuentes baada ya kuafikiana kutuma ofa nyingine kwa Azam FC!

KIGAMBONI YAPOKEA MSAADA WA MERIDIANBET… MUKWALA AKIRI KUWA NA DENI KUBWA SIMBA