Home Habari za Yanga Leo CLEMENT MZIZE ANAHITAJIKA ZAIDI WYDAD…WAARABU HAWAJAKATA TAMAA

CLEMENT MZIZE ANAHITAJIKA ZAIDI WYDAD…WAARABU HAWAJAKATA TAMAA

HABARI ZA YANGA-MZIZE

KLABU ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco haijaondoa Kabisa uwezekano wa Kupata Saini ya Clement Mzize ingawa Yanga Africa hawapo tayari kufanya hii Biashara sasa hivi

Kocha Mkuu wa Wydad Casablanca ambae ni Raia wa South Africa, Rhulani Mokwena ni Mshabiki wa Kutupwa wa Clement Mzize na ana shauku Kubwa ya kufanya nae Kazi.

Ripoti kutoka ndani ya Wydad Casablanca zinadai Rhulani Mokwena ameenda Mbali na kumfananisha Clement Mzize na Nahodha wa zamani Ivory coast na Legend wa Chelsea Didier Drodgba.

Rhulani nasema team ijayo Baada ya Yanga Africa ni Muhimu sana kwa ukuaji wa Kipaji Cha Clement Mzize.

Wydad Casablanca wanamthaminisha Clement Mzize mpaka USD250k na Rhulani Mokwena anamuona kama sehemu Muhimu ya Project yake kuelekea Kombe la Dunia la Vilabu 2025.

Kama ilivyo Kwa Rhulani , Kocha Mkuu wa Yanga Africa Master Miguel Angel Gamondi ni Shabiki namba Moja ya Clement Mzize na alishatoa msimamo wake Kwa Viongozi wa Yanga Africa kwamba hauzwi ingawa Kuna offer nyingi zikihitaji huduma yake.

Clement Mzize pia anatazamwa na Taifa Stars kama Mshambuliaji tegemezi kuelekea AFCON 2027 ambapo Tanzania itakuwa Mwenyeji pamoja na Kenya na Uganda.

SOMA NA HII  STRAIKA LA MAGOLI YANGA KUJIUNGA KARIBUNI