Home Uncategorized BARCELONA YACHAPWA 3-1 NA REAL MADRID, ANSU ATUPIA

BARCELONA YACHAPWA 3-1 NA REAL MADRID, ANSU ATUPIA


 ANSU Fanti kinda mwenye miaka 17 anayekipiga ndani ya Barcelona leo amepachika bao kwenye El Clasico kwenye mchezo wa La Liga wakati wakilala kwa kufungwa mabao 3-1 na Real Madrid. 


Ansu alipachika bao hilo dakika ya 8 akisawazisha bao lililopachikwa na Federico Valverde wa Real Madrid mwenye miaka 22 dakika ya 5 na bao la pili lilipachikwa na Sergio Ramos mwenye miaka 34 kwa mkwaju wa penalti.

Bao la tatu Barcelona ikiwa na staa wake Lionel Messi ilishuhudia  likipachikwa dakika ya 90 na Luka Modric mwenye miaka 35.

Ushindi wa leo wa Real Madrid umebebwa na uwezo wa nyota wao huku Barcelona kinda Ansu akifanya yake licha ya timu yake kupoteza pointi tatu muhimu kwenye mchezo uliochezwa ndani ya Uwanja wa Camp Nou.

Matokeo hayo yanaifanya Barcelona kuwa nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi tano na pointi zake ni saba huku Real Madrid ikiwa nafasi kwanza na pointi 13 baada ya kucheza mechi sita ndani ya La Liga.

SOMA NA HII  KLOPP HAELEWI CHA KUFANYA KUHUSU NAFASI YA ULINZI