Home Uncategorized YANGA YAIPIGIA MATIZI YA MWISHO KMC LEO

YANGA YAIPIGIA MATIZI YA MWISHO KMC LEO


 KIKOSI cha Yanga leo Oktoba 24 kimefanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa kesho Oktoba 25 dhidi ya KMC.


Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba saa 10:00 jioni.

Yanga imetua Mwanza leo na kupokelewa na mashabiki wake na imewakuta wenyeji wao KMC ambao waliwasili Mwanza Oktoba 22.

Yanga inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wake uliopita wa ligi mbele ya Polisi Tanzania kwa ushindi wa bao 1-0.

Inakutana na KMC ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na rekodi za miamba hii inapokutana uwanjani kuwa na ushindani mkubwa.

Msimu uliopita kwenye mchezo wao wa mwisho walipokutana Uwanja wa Uhuru, KMC ilishinda bao 1-0 na ule wa awali waliokutana Uwanja wa Uhuru ubao ulisoma 1-1.
SOMA NA HII  MUANGOLA HUYU AINGIA ANGA ZA YANGA