Home Habari za Yanga Leo STRAIKA LA MAGOLI YANGA KUJIUNGA KARIBUNI

STRAIKA LA MAGOLI YANGA KUJIUNGA KARIBUNI

HABARI ZA YANGA

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga Princess, Sabina Thom anatarajiwa kujiunga na kambi ya timu hiyo baada ya kumaliza fainali za Klabu Bingwa Afrika kwa Wanawake.

Yanga Princess imemsajili straika huyo kwa mkataba mmoja akitokea TP Mazembe ya DR Congo iliyofuzu kucheza fainali hizo za CAF,  hivyo hawezi kujiunga na wenzake kwa sasa hadi zimalizike.

Yanga tayari imeingia kambini kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) ambayo itaanza mwezi huu ikitanguliwa kwa mechi ya nusu fainali dhidi ya Simba Queens kuanzia Septemba 24 hadi 27.

Msimamizi wa mchezaji huyo (jina tunalo), amesema ataendelea kucheza TP Mazembe hadi itakapoishia kwenye michuano hiyo kwa mkataba maalumu.

“Tayari kasaini Yanga, lakini Mazembe wamemuazima baada ya kuona watashiriki CAF hawana mchezaji ambaye ana muunganiko, hivyo akirudi kutoka huko ndiyo atajiunga na timu,” amesema msimamizi huyo.

Alipotafutwa meneja wa timu hiyo, Kibwana Matokeo amesema: “Kwa sasa tunajiandaa na msimu mpya mambo mengine unajua usajili una mambo mengi sana.”

Mshambuliaji huyo siyo mara ya kwanza kucheza Tanzania kwani msimu 2021/22 aliwahi kuitumikia Simba Queens.

SOMA NA HII  INJINIA HERSI...AZIZ KI NI GHALI ZAIDI YANGA