Home Habari za Yanga Leo INJINIA HERSI…AZIZ KI NI GHALI ZAIDI YANGA

INJINIA HERSI…AZIZ KI NI GHALI ZAIDI YANGA

Habari za Yanga leo

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema Stephan Aziz Ki ndiye mchezaji ghali zaidi katika kikosi cha Yanga.

Raia huyo wa Burkina Faso alisajiliwa klabuni hapo Julai 2022 akitokea Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.

“Mkataba ni siri lakini niseme tu, Azizi Kl ndiye mchezaji ghali zaidi ndani ya Yanga Sc,” amesema Eng. Hersi Said.

Msimu uliopita Aziz Ki alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC,  akifunga mabao 21, huku akitwaa pia tuzo ya mchezaji bora wa Ligi MVP.

Hadi sasa nyota huyo mwenye ushawishi mkubwa Yanga, ana mchango mkubwa zaidi kwenye mafanikio ya Yanga kwa misimu miwili nyuma na dalali zimeonekana kwa msimu huu pia.

SOMA NA HII  NGOMA AWAPATA JEURI VIONGOZI WA SIMBA, SIRI YAFICHUKA...YANGA WAPIGWA ZA USO