Home Meridianbet KIGAMBONI YAPOKEA MSAADA WA MERIDIANBET…

KIGAMBONI YAPOKEA MSAADA WA MERIDIANBET…

meridianbet

Wataalamu wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet leo imefanikiwa kufika eneo la Kigamboni jijini Dar-es-salam na kuendelea na utaratibu wao wa kurudisha kwenye jamii ambayo imewazunguka.

Kama ambavyo wamezoeleka kurudisha kwenye jamii leo tena wamehakikisha wanaisaidia jamii ambayo ina uhitaji, Kwani leo wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa familia kadhaa katika eneo la Kigamboni mahitaji hayo ni kama mafuta, sukari, mchele, sabuni, pamoja na unga.

Meridianbet wameyafanya hayo katika kuuadhimisha siku ya Utu duniani ambayo hufanyika kila mwaka Agosti 19, Hivo wao wamehakikisha wanarejesha kwenye jamii ambazo zina uhitaji ili kwenda sambamba na wiki hii ya Utu duniani.

Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa baada ya EPL kurejea ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko kutoka Meridianbet Bi Nancy Igram aliongoza zoezi hilo na kufanikiwa kuzungumza machache “Kama inavyofahamika leo tunaadhimisha siku ya Utu duniani na sisi tumeamua kuuonesha Utu wetu kwenu na ndio maana tumefika hapa leo kujumuika na nyie kwa kutoa mahitaji haya muhimu kwenu”

Aidha familia ambazo zimeweza kupokea msaada leo kutoka kwa Meridianbet hazikuacha kutoa shukrani kwa mabingwa hao wa michezo ya  kubashiri na kusema makampuni, taasisi zingine zinapaswa kufanya kama ambavyo wamefanya Meridianbet kwa kuzikumbuka jamii zenye uhitaji.

SOMA NA HII  TUMIA KARATA 8 ZA KIPEKEE KUJIHAKIKISHIA USHINDI KUPITIA BLACKJACK LIVE YA MERIDIANBET...