Home Habari za Yanga Leo KOCHA VITAL’O AIONYA YANGA LEO

KOCHA VITAL’O AIONYA YANGA LEO

HABARI ZA YANGA

Kocha Mkuu wa Vitalo FC Sahabo Parris amesema klabu yake imejiandaa vilivyo kupambana na Yanga SC katika Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Katika mkutano na waandishi wa habari leo, amefahamisha kuwa anawaheshimu Yanga SC kwani ni timu yenye wachezaji wenye uchu wa kufanya vizuri.

Hata hivyo, amebainisha kuwa hakuna mechi rahisi katika Mashindano ya klabu Bingwa barani Afrika lakini ana matumaini ya kufanya vizuri dhidi ya wana Jangwani.

Vital’O FC ndiyo timu yenye historia kubwa nchini Burundi baada ya kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka wa 1992 ikiwa na Makombe 21 ya Ligi Kuu Burundi.

SOMA NA HII  YANGA WAFANYA KWELI KWA RANGA...GSM AONYESHA UMWAMBA...WAMZUIA KUTUA UARABUNI KIMAFIA...