Home Habari za Yanga Leo MVP AZIZ KI ATUMA SALAM SIMBA…AGOSTI 8 KWA MKAPA

MVP AZIZ KI ATUMA SALAM SIMBA…AGOSTI 8 KWA MKAPA

HABARI ZA YANGA

MOST Valuable Player (MVP) wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 Stephenie Aziz Ki ameweka wazi kuwa kila baada ya mchezo mmoja kinachofuata ni maandalizi kwa mchezo ujao ndani ya uwanja.

Ikumbukwe kwamba Yanga iliweka kambi Afrika Kusini ambapo ilialikwa kwenye mashindano maalumu ilitwaa Kombe la Toyota kwa ushindi wa mabao 4-0 baada ya dakika 90.

Katika mchezo huo Aziz alifunga mabao mawili, Clement Mzize alifunga bao moja na Prince Dube yeye alifunga bao moja la ufunguzi kwenye mchezo huo.

Agosti 4 2024 Yanga ilikuwa ni Wiki ya Wananchi ilipocheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Red Arrows ikapata ushindi wa mabao 2-1 na Aziz Ki alifunga bao moja kwenye mchezo huo.

Ki amesema: β€œKila baada ya mchezo tunaangalia kile ambacho kinafuata mbele, tulicheza nao kwenye Ngao ya Jamii ilikuwa ni wakati uliopita na sasa kwenye mpira tunazungumzia leo hivyo muhimu ni maandalizi mazuri ili kufanya vizuri.”

SOMA NA HII  VIGOGO TFF WAFICHUA 'MADUDU' YA FEI TOTO....AAMBIWA ATAJE TIMU ANAYOTAKA KWENDA JAMBO LIISHE...