Home Habari za Simba Leo TULIKAA KINYONGE SANA…MUDA WA KUFURAHI NA KUNUNA UMERUDI…LIGI KUU YA MOTO

TULIKAA KINYONGE SANA…MUDA WA KUFURAHI NA KUNUNA UMERUDI…LIGI KUU YA MOTO

HABARI ZA YANGA

Sasa kazi inaanza rasmi. Ligi Kuu Bara inaanza leo Ijumaa, lakini kesho kuna mechi nyingine nne za ligi hiyo ukiwamo ule wa Simba dhidi ya Tabora United sambamba na michezo ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika. Lakini hata katika Klabu Bingwa kwa nchi za Cecafa nako ‘game on’ huko Ethiopia.

Yanga, Azam FC na Coastal Union ambazo hazitacheza mechi za Ligi Kuu kwa wikiendi hii, zenyewe zipo bize na mechi za raundi ya kwanza, kama itakavyokuwa kwa wawakilishi wa Zanzibar, JKU na Uhamiaji, huku mnyama akisubiri hadi raundi ya pili ya michuano hiyo ya ubingwa wa Afrika kwa ngazi za klabu.

Simba Queens ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Cecafa kusaka tiketi ya Klabu Bingwa Afrika itakuwa uwanjani keshokutwa Jumapili dhidi ya FAD ya Djibouti, licha ya michuano hiyo kuanza rasmi leo ikishirikisha klabu tisa tofauti zilizofangwa makundi mawili.

Wakati Simba ikianza kuliamsha katika Ligi Kuu, vigogo wenzake, Azam FC, Yanga pamoja na Coastal sawia na JKU na Uhamiaji za Zanzibar zenyewe zitakuwa na kibarua cha mechi za kimataifa, wakati zitakapotupa karata ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho zikiwa nyumbani na ugenini. Mechi hizo za kimataifa zinaanza rasmi Ijumaa hii, lakini kwa wawakilishi wa Tanzania kazi itaanza rasmi kesho.

Yanga ndiyo itakayokata utepe kwa anga hizo kwa kucheza na Vital’O ya Burundi ambao ndio wenyeji kwenye Uwanja wa Azam Complex, kuanzia saa 10:00 jioni kabla ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union inayorejea katika michuano hiyo tangu 1989, itakuwa ugenini kuvaana na Bravos do Maquis ya Angola saa 12:00 jioni, kisha ngoma nyingine tatu zitapigwa Jumapili, Uhamiaji ikiamsha mapema.

Uhamiaji ambao ni wenyeji wa mchezo huo itakuwa Libya kupepetana na Al Ahli Tripoli kuanzia saa 9:30, alasiri katika mechi ya Kombe la Shirikisho, kabla ya Azam na JKU kufuata katika Ligi ya Mabingwa.

Azam itakuwa wenyeji wa APR ya Rwanda kuanzia saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, kabla ya JKU itakuwa wenyeji wa Pyramids ya Misri mechi itakayopigwa jijini Cairo saa 2:00 usiku timu hizo zikitesti zali baada ya kuchemsha msimu uliopita katika Kombe la Shirikisho zikitolewa raundi za mapema.

JKU ilitolewa na Singida BS, wakati Azam iling’olewa na Wahabeshi wa Bahir Dar Kenema kwa njia ya matuta na safari hii zinatesti zali katika Ligi ya Mabingwa ambao Yanga chini ya Gamondi iliweka rekodi kwa kuingia makundi baada ya kupita miaka 25 tangu ilipofanya hivyo mwaka 1998 na kwenda hadi robo.

Safari hii Yanga ikiwa na mziki mnene wa nyota waliokuwa msimu uliopita na wale waliongezwa akiwamo Clatous Chama, Jean Baleke, Duke Abuya wazoefu wa michuano hiyo sambamba na kina Chadrack Boka na Abubakar Khomeiny wana kiu ya kuisimamisha Vital’O ambao sio wageni kwa soka la Tanzania.

SOMA NA HII  BAADA YA KUCHAPWA JANA...INJINI HERSI 'CHAP HARAKA' AITA MKUTANO WA WANACHAMA YANGA...AJENDA HIZI HAPA..