habari za simba
Habari za Simba Leo

AHMED ALLY ATOA KAULI HII…BAADA YA SIMBA KUFANYIWA VURUGU

Abubakar September 16, 2024 2:59 pm

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba, Ahmed Ally  amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa timu yao iko salama licha ya ‘purukushani’ zilizojitokeza uwanjani baada ya mchezo dhidi ya Al Ahly Tripoli uliopigwa jana huko Libya

Baada ya mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana, mashabiki wa Al Ahly Tripoli walifanya vurugu uwanjani kwa kuwarushia chupa wachezaji wa Simba pamoja na waamuzi

Ahmed amesema timu ililazimika kukaa uwanjani kwa takribani dakika 40 kabla ya kupanda basi kuelekea hotelini

“Tunashukuru tuko salama pamoja na vurugu zilizojitokeza, tumerejea hotelini salama kabisa”

“Baada ya mchezo kumalizika vurugu zilijitokeza uwanjani, maafisa usalama walitushauri tuende vyumbani tusubiri mashabiki waondoke uwanjani ndipo nasi tuondoke”

“Hivyo tulikaa uwanjani kama dakika 40 ndipo tukapanda basi kuelekea hotelini. Kulikuwa na tukio la golikipa wetu Aishi Manula kushambuliwa wakati tunatoka jukwaani kuelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo, lakini tunashukuru nae hakupata madhara yoyote”

“Manula alishambuliwa na moja ya maafisa wa usalama katika tukio la kushangaza kwani ni wao waliotushauri tuende katika vyumba vya kubadilishia nguo tusubiri vurugu zutulie,” alisema Ahmed

Simba inatarajiwa kuondoka leo kurejea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ambao utapigwwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumapili ijayo.

AZIZ KI AWAITA MASHABIKI ZANZIBAR…ANAZITAKA DAK 90 CHEZA TEEN PATTI POKER, UPIGE MKWANJA KIRAHISI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

One response to “AHMED ALLY ATOA KAULI HII…BAADA YA SIMBA KUFANYIWA VURUGU”

  1. […] ya pili katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, kocha mkuu wa JKT Tanzania, Ahmed Ally amezipa mbinu timu […]