Home Habari za Yanga Leo AZIZ KI AWAITA MASHABIKI ZANZIBAR…ANAZITAKA DAK 90

AZIZ KI AWAITA MASHABIKI ZANZIBAR…ANAZITAKA DAK 90

Habari za Yanga leo

KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz KI amesema bado hawajamaliza kuna dakika 90 nyingine pale New Amaan visiwani Zanzibar.

Yanga imewasili jijini Dar es Salaam ikitokea Ethiopia, ambapo walicheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE jana Jumamosi, Septemba 14.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Abebe Bikila, Yanga iliondoka na ushindi wa 1-0, bao likifungwa na mshambuliaji Prince Dube.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuwasili nchini, Aziz alisema licha ya kupata ushindi ugenini anaamini mechi ya nyumbani itakuwa bora zaidi kwa upande wao.

Aliongeza kuwa kwao muhimu ni kucheza ardhi ya nyumbani haijalishi wapo Azam Complex kwani kipaumbele chao ni kushinda.

“Muhimu kuja kucheza Tanzania iwe Amaan Zanzibar au Azam Complex Chamazi tuko nyumbani kazi yetu kucheza na kuhakikisha tunashinda mchezo hilo ndio muhimu,” alisema Aziz KI

Mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya CBE umepangwa kuchezwa Septemba 21, Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja, Zanzibar.

SOMA NA HII  INJINIA HERSI...AZIZ KI NI GHALI ZAIDI YANGA