Home Habari za Yanga Leo SIO TU AZIZ KI, PACOME ANA BALAA LAKE.

SIO TU AZIZ KI, PACOME ANA BALAA LAKE.

HABARI ZA YANGA

MASHABIKI wa Yanga wamekuwa wakiliimba sana jina la Stephane Aziz KI ndiye nyota hatari katika kikosi hicho kutokana na msimu uliopita kuibuka Mfungaji Bora akiwa na mabao 21 na asisti nane, lakini straika wa zamani wa timu hiyo aliyepo Singida BS, Joseph Guede amemtaja Pacome Zouzoua akisema ndiye mchezaji tishio zaidi.

Guede aliyecheza na nyota hao wa Yanga msimu uliopita baada ya kusajiliwa kupitia dirisha dogo, alisema kwamba Yanga ina mastaa wengi lakini Pacome Zouzoua ndio mchezaji tishio na bora ambaye alikuwa akifurahia kucheza naye ndani ya kikosi cha timu hiyo sasa ni mpinzani na mchezaji wa kumhofia.

Pacome licha ya wengi kumuona sio tishio lakini kiuhalisia ni moja ya injini muhimu sana pale kwenye kiungo cha Yanga.

Moja kati ya mchezaji hatari zaidi anapokuwa na mpira mguuni, Hujui atafanya nini kwa wakati gani, lakini hata asipokuwa na mpira sio mchezaji wa kukaa sehemu moja, ni aina ya wachezaji wasioonekana “Invisible Player” wakiwa uwanjani ili kumkaba unahitaji atembee na mchezaji kila eneo la uwanja.

SOMA NA HII  FADLU, AHOUA WATAMBA TUZO ZA MWEZI AGOSTI