Mnyama Simba anatupa karata muhimu leo akihitaji ushindi wa aina yoyote dhidi ya Al Ahli Tripoli ili itinge hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo huo utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa au kwa Lupaso majira ya saa 10:00 Jioni.
Tayari Walibya walioonyesha kuingiwa ubaridi mapema tangu walipokuja nchini kwa kuweka ulinzi wa mabaunsa na kukimbilia katika ubalozi wa nchi hiyo kama kujihami pengine kwa kile kilichofanywa na mashabiki wao wiki iliyopita kuwafanyia fujo Wekundu hao baada ya kutoka suluhu.