Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAETHIOPIA….GAMOND AANZA KUTAFUTA CD ZA ‘KONEKSHENI’…

KUELEKEA MECHI NA WAETHIOPIA….GAMOND AANZA KUTAFUTA CD ZA ‘KONEKSHENI’…

Habari za Yanga leo-Miguel Gamondi

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema haifahamu CBE AS ya Ethiopia na analazimika kutafuta CD za michezo yao kuwafatilia na watu gani wa kuchungwa pamoja na aina ya mchezo wanaocheza.

Amesema anapaswa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wao wa hatua ya pili ya kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE AS ya nchini Ethiopia.

Gamondi amesema muda wa maandalizi wa mchezo huo mdogo na anaimani timu zote zilizoingia hatua hiyo ni bora na kuhitaji kuanza kuwafatilia wapinzani wao hao mapema kabla ya kukutana nao.

Amesema licha ya kuwepo na kibarua cha ligi kuu Tanzania lakini lazima kupata taarifa za CBE AS, kufahamu ubora wa kila eneo kuanza safu ya ulinzi, viungo na mabeki.

” Siifahamu timu ya CBE SA ila tunapaswa kupata matokeo mazuri Ethiopia na tuje tufuzu tukiwa hapa Tanzania, nimeanza kufanyia kazi, kuwafatilia wapinzani wetu, tunahitaji kuwa imara na kufahamu tunacheza ni timu ya aina gani,” amesema Gamondi.

Ameeleza kuwa ana kazi kubwa ya kuandaa timu yake kuelekea mchezo huo kwa sababu ya kutokuwepo kwa muda na wachezaji wake 14 wameitwa na timu zao za Taifa wakati ambao wanahitaji kusahihisha makosa yao.

Wachezaji wa Yanga walioitwa katika timu za Taifa ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Clemete Mzize, Ibrahim Bacca, Nickson Kibabe, Mudathiri Yahya na Abdultwalib Mshery. Djigui Diara, Kennedy Musonda, Clatous Chama, Stephane Aziz Ki, Prince Dube na Duke Abuye.

“Muda sio rafiki wachezaji 14 wapo kwenye majukumu ya timu zao za Taifa, wanarudi siku mbili hadi tatu kabla ya mechi, sijapata muda wa kuandaa timu yake na tunalazimika kushinda mchezo wetu wa ugenini,” amesema kocha huyo anayelia na kalenda ya Shirikisho la Soka Afrika.

Ameongeza kuwa wachezaji wanasafiri sana, wanacheza mechi nyingi, mfano wao wanacheza Ethiopia, nyota wake wataenda lakini sio kwa muda sahihi ambao angepata kufanyia kazi mapungufu yake ikiwemo matumizi ya nafasi wanazotengeneza.

Gamondi amesema wamekuwa shida ya kutumia nafasi ndani ya kipindi cha kwanza, kilichokotea wanarudi uwanja wa mazoezi kukifanyia kazi ili kuwa imara kwenye mechi zinazofuata.

SOMA NA HII  NJIA YA MIQUISSONE KURUDI SIMBA YAZIDI KUWA NYEUPE....KAIZER CHIEF WAAMUA KUMSUSA GHAFLA...