Home Habari za Simba Leo MWAMNYETO AKUBALI KUHITAJIKA SIMBA

MWAMNYETO AKUBALI KUHITAJIKA SIMBA

Habari za Yanga leo

NAHODHA wa Yanga SC Bakari Mwamnyeto amethibitisha kuwa ni kweli klabu ya Simba SC ilimuhitaji kumsajili kwaajili ya kujiunga na kikosi chao katika msimu huu mashindano wa 2024- 2025.

“Viongozi wa Simba SC walikuwa wanaongea na Meneja wangu kwa muda wote lakini mimi ni mchezaji natafuta maisha kwahiyo sehemu yoyote mambo yakienda vizuri nacheza” amesema Bakari Mwanyeto Nahodha wa Yanga SC.

Katika dirisha kubwa baada ya Simba kumsajili Lameck Lawi walikuwa wanapushi sana kuipata saini ya Mwamnyeto, lakini mambo yakaenda kombo akaongezwa mkataba na Yanga huku akipewa mshahara mnono wa Mil 10.

Simba ili kutafuta mbadala wa Mwamnyeto waliamua kuingia sokoni haraka, ndipo walipompata kijana hatari Abdulrazak Hamza ambaye amekuwa na kiwango bora sana kwenye mechi alizopewa nafasi ya kucheza.

SOMA NA HII  MAYELE APEWA RUHUSU RASMI NA YANGA, HUYU HAPA NDIO MRITHI WAKE