Home Habari za Yanga Leo PRINCE DUBE AWAOMBA MSAMAHA…YANGA IKIVUNJA UTEJA WAO KWA WAHABESHI

PRINCE DUBE AWAOMBA MSAMAHA…YANGA IKIVUNJA UTEJA WAO KWA WAHABESHI

HABARI ZA YANGA-DUBE

BAO moja lililofungwa na Prince Dube dakika 45 kipindi cha kwanza dhidi ya CBE SA ya Ethiopia lilitosha kuitanguliza Yanga mguu mmoja mbele katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, huku ikivunja mwiko wa kutiopata ushindi katika ardhi ya nchi hiyo katika michuano ya CAF.

Ikicheza kwenye Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa, Yanga itajilaumu kwa kushindwa kutoka na ushindi mnono kutokana na kutengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia katika vipindi vyote vya mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa.

Dube, aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Azam FC, licha ya kutumia nafasi moja ya dhahabu kwa timu yake alishindwa kushangilia bao hilo badala yake aliomba radhi kwa benchi la ufundi kutokana na kushindwa kutumia nafasi nyingi alizozipata.

Nyota huyo wa kimataifa aliyeanzishwa sambamba na Stephane Aziz KI, Maxi Nzengeli na Pacome Zouzoua, huku eneo la kiungo likiwa chini ya Khalid Aucho na Mudathir Yahya alifunga bao hilo akipokea pasi kutoka kwa Aziz KI na kumchengesha kipa wa CBE kabla ya kufungwa eneo la juu.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kuhitaji sare yoyote katika mechi ya marudiano wikiendi ijayo itkayopigwa Uwanja wa New Amaan, Zanzibar ili kuandika historia ya kucheza makundi kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliopita ikiwa ni baada ya kupita miaka 25 tangu ilipocheza kwa mara ya kwanza 1998.

Ushindi huo ni muendelezo wa rekodi kwa Kocha Miguel Gamondi ambaye ndiye aliyeipeleka Yanga makundi baada ya miaka 25 na kuishia robo fainali, baada ya awali kuvunja mwiko wa Al Merrikh ya Sudan waliyoifunga raundi ya pili kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda ugenini 2-0 na nyumbani 1-0.

Rekodi zinaonyesha Yanga haijawahi kuifunga timu kutoka Ethiopia ikicheza nyumbani kwao, kwani mechi nne zilizopita ilitoka sare mbili na kupoteza mbili ikiwamo mara ya mwisho mwaka 2018 ilipolala 1-0 kwa Welayta Dicha katika Kombe la Shirikisho, lakini ushindi wa nyumbani wa 2-0 ukaivusha kuingia makundi.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUCHAPWA JUZI...KIUNGO WA BAMAKO AITAJA YANGA NA MAYELE...ISHU NZIMA IKO HIVI...