Home Ligi Kuu BALAA LA LEO UWANJANI LILIKUWA NAMNA HII, MATOKEO HAYA HAPA

BALAA LA LEO UWANJANI LILIKUWA NAMNA HII, MATOKEO HAYA HAPA


 LEO Septemba 27, Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPL) imeanza na mechi tatu za kukata na shoka zimechezwa na mwisho wa siku kila mmoja akapata kile ambacho alikipanda.

Kwa Mtibwa Sugar leo wameambulia maumivu wakiwa uwanja wao wa nyumbani, Mabatini baada ya kuonja joto ya jiwe kutoka kwa Mbeya Kwanza.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa ufunguzi umeshuhudia bao la kwanza msimu wa 2021/22 likipachikwa na Edger William ambaye alijikunjua akiwa ndani ya 18 ilikuwa ni dakika ya 49.

Mchezo mwingine ulikuwa ni ule wa Coastal Union 1-1 Azam FC ambapo ulichezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ni bao la Daniel Amoah wa Azam FC alipachika bao hilo dakika ya 82 na liliwekwa sawa na nyota Hance Masoud dakika ya 89.

Mchezo mwingine uliochezwa leo ni ule wa Namungo 2-0 Geita Gold ambapo ni Shiza Kichuya alipachika bao la kwanza dakika ya 13 na lile la pili lilifungwa na Reliat Lusajo dakika ya 89.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMCHEZEA RAFU MBAYA KAPOMBE...MAKAME AJITETEA..ADAI ALIKUWA ANATIMIZA WAJIBU...