Habari za Yanga Leo

SI MLISEMA WAZEE…KAZI IMEANZA YANGA

Abubakar October 3, 2024 8:31 pm

MABINGWA watetezi wa Ligi kuu ya NBC, klabu ya Yanga SC hii leo imeibuka na ushindi mnono wa bao 4-0, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kuanza kwa msimu mpya wa Ligi.

Yanga imecheza na Pamba Jiji ya Mwanza, ambao walianza mchezo vizuri wakitanguliwa kwa bao 1 la kichwa kutoka kwa Ibrahim Bacca.

Baada ya Hapo Walipata kadi nyekundu na ndipo Yanga wakapata nafasi ya kuanza kutupia mipira nyavuni.

Magoli ya Yanga yalifungwa na Ibrahim Bacca, Aziz Ki kwa mkwaju wa penati, Maxi Nzengeli na Kennedy Musonda aliyeingia kutokea sub.

Yanga inafikisha alama 12 ikiwa sawa na Simba lakini inazadiwa kwa mabao ambapo, Simba amefunga mabao 9 huku Yanga akiwa na mabao 8.

Kesho pia Mnyama Simba anatarijia kushuka dimbani, kuwakaribisha wana mangoshi wagosi wa kaya Coastal Union.

SIMBA BAADA YA USAJILI WAITAKA ROBO FAINALI KISA KAGOMA …AHMED ALLY “ATUPA JIWE JEUSI KWENYE SHIMO LA KIZA”….