Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele mwenye kumbukumbu nyingi nzuri katika ardhi ya Tanzania, ameshindwa kujizuia kwa kueleza miongoni mwa vitu ambavyo anavimisi kutoka kwa Stephane Aziz KI.
Mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu Bara 2022/23 alikuwa sehemu ya watazamaji ambao walijitokeza majuzi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na kuishuhudia Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mkongomani mwenzake, Max Nzengeli.
“Aziz Ki kuna vitu vingi.. vitu vingi navimisi ilikuwa kwenye mechi hivi nasumbuana naye. Wewe hunipi pasi sasa mimi ni straika ilikuwa lazima nifunge, vitu kama hivyo muda mwingine kwenye mpira vinatokea na mnaongea,” amesema Mayele.
“Nampongeza sana kwa kuwa mfungaji bora msimu uliopita, ni ngumu kwa namba kumi lakini yeye ameweza, msimu huu nao pia akiendelea, apambane atafanya vizuri tu.”
Mayele ambaye alipewa zawadi ya jezi na Aziz Ki mara baada ya wawili hao kukutana, amesema alipotua Tanzania siku moja kabla ya mechi hiyo akitokea Hispania kwa mapumziko, alifanya mawasiliano na fundi huyo wa Burkinafso ambaye alimsaidia kuwa mfungaji bora katika msimu wake wa mwisho akiwa na Wananchi na kumweleza atakuwa Chamazi katika mchezo huo wa ligi.
“Nilivyomweleza alifurahi na kusema atanipa zawadi ya bao na jezi. Hakufunga, lakini jambo muhimu nimeona alivyokuwa msaada kwa timu,” ameongeza.
Mayele ambaye kwa sasa yupo nchini kwa mapunziko baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu Misri akiwa na Pyramids, alionekana akiingia uwanjani dakika chache kabla ya mchezo kuanza na wakati akiingia mashabiki wa Yanga walimpokea vizuri huku wakimpigia makofi.
Akiwa Misri msimu uliomalizika siku chache zilizopita, Mayele alishindwa kuwa mfungaji bora wa ligi baada ya kuzidiwa kete na mshambuliaji wa Al Ahly, Wessam Abou Ali.
Ali ametawazwa kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Misri akiwa na mabao 18 wakati Mayele akiwa na mabao 17. Huo umekuwa msimu mwingine kwa Mayele akikosa kiatu cha ufungaji bora dakika za mwisho.
Akiwa DR Congo, Mayele alikosa kiatu mbele ya Jean Baleke na msimu wa kwanza akiwa Yanga alikosa pia kiatu mbele ya George Mpole.
[…] watetezi wa Ligi kuu ya NBC, klabu ya Yanga SC hii leo imeibuka na ushindi mnono wa bao 4-0, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kuanza kwa msimu […]
[…] watetezi wa Ligi kuu ya NBC, klabu ya Yanga SC hii leo imeibuka na ushindi mnono wa bao 4-0, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kuanza kwa msimu […]